Watu wengi huishi kwa kile walichoambiwa na dunia – “Wewe si kitu,” “Wewe ni mdhaifu,” “Wewe ni kama baba yako.” Lakini ndani ya Kristo, tunapata utambulisho mpya. Tunazaliwa upya – na historia yetu haidhibiti tena hatima yetu.
Umeumbwa upya kwa Kristo – Usiishi kulingana na makosa ya zamani.
Wewe ni mrithi wa ahadi za Mungu – Warumi 8:17
Dhambi zako zimesamehewa kabisa – 1 Yohana 1:9
Una mamlaka mpya kiroho – Luka 10:19: “Nimewapa mamlaka…”
“Ee Mungu, nipe ujasiri wa kuishi katika utambulisho wangu mpya. Niondolee mawazo ya zamani na unijaze na ukweli wa Neno lako.”
Wewe si yule uliye kuwa. Wewe ni kiumbe kipya. Usiishi kama mfungwa – maisha yako mapya yameanza ndani ya Kristo.