Falsafa ya masomo –Hii ni shule iliyoundwa ili kumpatia mwanafunzi wa Neno la Mungu elimu ya Biblia kwa kina na mapana. Masomo yaliyopo ni yale yatekwayo kama maji kutoka kwenye Biblia. Masomo haya ni kwa ajili ya yeyote anayependa Neno la Mungu.
Tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika ibada zetu, mahali pa amani, upendo, na uwepo wa Mungu. Kanisa la Kristo Yesu Ulimwenguni ni familia ya waumini wanaomtumikia Mungu kwa Roho na kweli, wakijengwa na Neno lake, na wakipendana bila masharti.
Katika dunia yenye mgawanyiko na maumivu, upendo wa Kristo ndio daraja letu. Ni nguvu inayoshinda chuki, ni mwanga unaofukuza giza, ni mnyororo wa neema unaotufanya kuwa familia moja – bila kujali rangi, kabila, hali, au historia.