GLOBAL CHURCH OF CHRIST JESUS TANZANIA
IDARA YA UMISHENI NA ELIMU
Limeandaliwa na Willy Emmanuel
USIONDOKE KAMA ULIVYOKUJA
Marko 5:2-28
1. Kufungwa
2. Makubalini
3. Kulia
4. Kumkimbilia Yesu
UTANGULIZI
Pamoja na kwamba sio mji wa wayahudi na pamoja na dhoruba bado alidhamiria kwenda
Tuko katika dunia ambayo watu wa kanisani wanaenda waliko watu wa kanisani.
Katika sura iliyotangulia tunaona lililotokea na katika surah ii tunaona kwa nini ilitokea
* Sura hii inatuambia kwa nini kulitokea mawimbi baharini.
* Sura hii inatunambia kwa nini Yesu alingíangíania kwenda ambako atafukuzwa
Nikijua utanifukuza siwezi hata kukusalilmia
Yesu anaenda ambako hakuna ìamenî
Anaenda kwa makusudi na sio kwa ajili ya kundi bali kwa ajili ya mtu mmoja
Leo tuko juu juu kwa ajili ya kujali umati kubwa na tunapuuza mtu
Nimejifunza kwamba ukipenda watu utavutia umati
Lakini huwezi kuvuta umati kama hupendi watu kwa sababu upendo ni sumaku na inavuta tunaowapenda
Alipofika, alikutana na mtu aliyeishi makaburini. Hakuwa mzimu, hakuwa maiti bali mtu mwenye mapepo aliyekuwa anaishi makaburini
Mapepo yalimsihi sana Yesu ayaruhusu yawaingine nguruwe
Ndio maana tunajua hii haikuwa nchi ya Wayahudi maana Wayahudi hawafugi nguruwe badala yake wanafuga kondoo
Hayo ndio mazungmzo ya Yesu na mapepo. Mazungumzo ya mema na mabaya. Haya ni mazungumzo ambayo lazima uwe rohoni ndio unaweza kufanya mawasiliano na kusikia. Yesu kama roho anaziamuru roho chafu
Yesu anapokutana na mwenye mapepo mapepo huondoka.
Alipoyaruhusu kuwaingia nguruwe na mapepo yalipowaingia nguruwe nguruwe walitumbukia baharini, bahari ambayo Yesu amenusurika kuzama yakazama yenyewe na nguruwe
Sasa unaanza kuelewa kwa nini bahari ilitaka kumzamisha Yesu
Wanaotaka kukuzamisha watazama wenyewe! Tena watakuomba wasione mafanikio yako, watazama huku unawaangalia
Maji huwakilisa uhai kwa mwanadamu lakini ni kaburi kwa nguvu za giza
Dunia ilizaliwa kutoka kwenye maji
Watoto wanazaliwa kutoka kwenye maji
Wakati waovu wanazamishwa safina iliokoa nane kwenye maji
Waisraeli waliokoka kwa maji wakati Farao anazama kwenye maji
Kabla ya kuingia patakatifu kulikuwa na birika ya maji
Naamani aliambiwa akajichovye kwenye maji ya Yordani
Mtu hazaliwi kiroho bila maji na roho
Maji ni kaburi kwa sababu tunapobatizwa kwenye maji tunazikwa, tunauzika utu wa shetani
Mungu husafiha kanisa kwa neno katika maji
Mbele ya kiti cha enzi kuna bahari ya kioo
Pepop amtokapo mtu hupitia sehemu ambayo haina maji siku hiyo waliingizwa kwenye maji! Unadhani nini kilitokea
Kama unaona Yesu anayaruhusu mapepo yaingie kwenye nguruwe sasa unajua kwa nini
Nguruwe walikuwa 2,000 na mapepo yalikuwa ni jeshi (lejion) kikosi cha askari kuanzia 3,000-6,000. Kama mapepo yote yaliwaingia nguruwe 2,000 ina maana kila nguruwe aliingiwa na mapepo matatu.
Kama uliona Yule mtu akikata pingu na minyororo ni kwa sababu alikuwa na jeshi.
Sasa unajua kwa nini
Wachungaji wa nguruwe walikimbia- siwalaumu
Wanyeji walipokuja na kumkuta aliyekuwa na amepona na ametulia ni kama anasema ìhey habari gani?î
Akiwa amevaa nguo na akili timamu. Kufunguliwa kwake kuliwatisha
Hivi unajua kwamba wanaofurahia mateso yako ni wale wanaokufunga
Kufunguliwa kwako kunawatisha sana, Shetani anatishika, Kuzimu inatetemeka
Kanisa limefungwa mno kiufahamu, ukijaribu kulifungua kanisa kuna watu wanatishika
Hakuna aliyefurahia kufunguliwa kwake
Watu wanakuwa na amani ukiendelea kufungwa, ni kufunguliwa ndiko kunakowatisha
Mapepo yalimsihi Yesu, naoo wanamsihi Yesu aondoke. Hicho ndicho walichofanya! Walimfukuza Yesu badala kumsihi akae nao
Kwanini?
Nawaza kwanini pia?
Kwanini nguruwe walikuwa wanalishwa makaburini ambako analala mwenye mapepo?
Umejua kwa nini walimfukuza Yesu?
Ngoja niendelee, kwanini Yesu aliyakubalia mapepo yawaingine nguruwe? Kwanini awe tayari kusababisha hasara? Utajua kwanini utakapojua kwa nini Farao anapofuata vyombo walivyoazima waisraeli alizamishwa
Kuna watu wananufaika na kuugua kwako
Kuna ndugu wanakuvuruga ili wachume utajiri
Kuna watu wananufaika unapodhalilika
Familia yako haieleweki lakini kuna watu wananufaika
Unajiuliza kwanini, ndio maana Yesu alimwambia aende nyumbani kwao kwa ndugu zake! Akwahubirie alitendewa
Kwani kwao kulikuwa ni wapi, ni kule walikotoka waliomfukuza Yesu au ni kwingine? Ili ujue hili jiulize kwa nini alitaka kwenda na Yesu na sio kwenda kwao
Kama Yesu alimfungua mwenye mapepo 6,000 atashindwa kukufungua?
Mwambie uliyekuja naye, ìusiondoke kama ulivyokuja.
Mwisho wa Utangulizi:
Baba Mungu katika Jina la Yesu, Litakase neno hili katika mioyo ya watu wako
Nakushukuru kwa yale uliyptuandalia, pita katikati yetu Bwana.Naamini utatufungua,naamini utatukomboa, naamini utatuponya
Utaturejesha, Utatufanya upya na hatutaondoka kama tulivyokuja
Katika Jina La Yesu!
Amen.
Wanadamu ni nafsi tatu na hali hiyo inatufanya tuwe katika hali isiyotabirika
Sisi ni roho, sisi sio mwili.
Sisi ni roho tuna nafsi yenye akili, kumbukumbu na hisia na tunaishi kwenye mwili
Sisi ni roho, tuna nafsi, tunaishi kwenye mwili lakini hatuihi mwilini
Ndio maana Paulo anasema nyumba iliyo ya maskani hii ikiharibika nina jingo lingine
Kwa maneni mengine, kifo hakiondoi uhai kifo kinahamisha uhai kwenda kwenye jingo lingine
Mimi sio mwili ila naishi kwenye mwili. Utu wangu wa nje (mwili) unaponyauka kama majani ya mtini utu wangu wa ndani unafanywa upya
Unaweza kupima typhoid kkumbe tatizo liko rohoni ila linaonekana mwilini.
Unaweza kuwa na kitu kinachohambulia utu wako wa ndani lakini lakini dalili zikaonekana mwilini
Ayah ii inashughulika na yote matatu na nataka ujue kwamba jambo moja huathiri lingine
Umewahi kujiuliza kwanini kuna wakati unashindwa kupata usingizi?
Unachukua dawa za usingizi. Dawa za usingizi zimetengenezwa kwa ajili ya mwili na tatizo lako liko kichwani
Tatizo tunalolisoma hapa ni kwamba walikuwa wanajaribu kulidhibiti tatizo la kiroho kwa kutumia kamba za kimwili.
Tatizo lake lilikuwa linaumiza mwili wake pia
2Na alipokwisha kushuka katika mashua, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;
Unafungaje pingu roho?
Walikuwa wanatibu dalili na sio chanzo.
Najiuliza kama tunatibu dalili au chanzo cha Kanisa kurudi nyuma?
Je tunafanya maombi ili tuwe nafuu kwa nje wakati chanzo kipo ndani/
Mfano; watu wanene mara nyingi wanaugua kisukari kwa hiyo wanaepuka baadhi ya vyakula, lakini inawezekana sicho unachokula bali kinachokutafuna ndicho kinachokufanya uwe mnene. Kwa hiyo ukitibu inarudi tena
Huu ni wakati wa kwenda ndani ya dalili na kushuhgulikia chanzo.
Ili unielewe vizuri na upate ujumbe wako kwenye aya hii ni kwamba ni lazima ukubali kwamba inawezekana unayemchukia unamchukia kimakosa.
Kwa sababu unaangalia tu alichofanya sio kwa nini alifanya alichofanya na unaweza ukawafanya wasiwe vile unavyotamani kwa nini unaendelea kufanyia kama wakosaji
Maudhui ya aya hii ni WANNE WANAONDOSHWA
Najaribu kuchimba aya hii
1. Walimwondosha mwenye mapepo kutoka kijijini
2. Yesu aliyaondosha mapepo
3. Yesu alimwondosha makaburini aliyekuwa na mapepo
4. Wenyeji walimwondosha Yesu kutoka kwao, kutoka makaburini
Heri Yesu akuondoshe leo kutoka mabaurini, ukahubiri
Mathayo 28:18-20
Kuna watu bila kujali na bila kukusikiliza watakufukuza kwenye maisha yao.
Watakutenga kwa sababu wako kwenye nafasi ambayo hakuna anayeweza kuwatenga
Angeshuka Mungu kufanya tathimini kati yenu wao ndio wangetengwa.
Mungu anataka kukuondosha kutoka makaburini ambako ndugu zako na rafiki zako walikuacha ufie huko
Tunapoisoma aya tunaona mtu mwenye ndugu na marafiki ni mkiwa, ni wa mitaani kwa sababu baadaye tunaona Yesu anamwambia aende nyumbani kwa jamaa zake
Jamaa zake ni ndugu zake au rafiki zake
Kama una marafiki unawezaje kuishia makaburini. Hapa mwenye ndugu anaishi makaburini
Ukweli ni kwamba, hata marafiki wanachoka!
Hata ndugu wanachoka
Kuna marafiki waliochoka hapa?
Kuna ndugu waliochoka hapa?
Jihadhari usichoshe marafiki
Jiepushe usichoshendugu
Kila siku wewe tu wewe tu, matatizo yako kla siku unawamabia watu wala hakuna siku unawambia neno la Baraka!
Hata upendo unachoka! Hata watoaji na wafadhili wanachoka. Usiruhusu mtu azidishe kukusaidia, kitakachotokea watachoka na kukuacha makaburini
Yule mtu anaishi makaburini ambako tunawaacha tunaowapenda
Japokuwa hajafa bado, walimwacha makaburini, sio tu aliachwa makaburini bali na upendo wao kwa Yule mtu ulikuwa umekufa uliachwa makaburini
Walimwacha kule ajifie, ila alikuwa hajafa. Kama unaniacha makaburini huku umenifunga kwa pingu na minyororo unataka nife
Laiti wasingemfunga ili angalau ajitafutie chakula
Lakini ukinitupa kaburini huku umenifunga unasubiri nife halafu unashangaa nikizikata pingu na minyororo-nataka niishi
Unashanga kwanini unanikuta milimani ñSitaki kufia makaburini
Siwezi kufanana na yanayonizunguka kwenyemaisha yangu-nitakata pingu na minyororo yao.
Nitaenda milimani nitafakari kwa maumivu kwa nini niliowathamini kama ndugu wamenitupa
Kwanini niliowathamini kama rafiki wameniacha makaburini nife peke yangu
Naumia, sioni thamani yangu duniani, najichukia, najichoma, najikata
Bora nife kwa kujikata mwenyewe na mawe kuliko kufia makaburini
Jambo moja ninalojua ni kwamba wanavyochukulia walivyonitupa makaburini ni tofauti na ninavyojichukulia
Sijafa bado!
Ukiishi na walio kaburini sio muda unakuwa kama wao.
Waambie sijafa bado!
Kuna watu wanasubiri upige magoti ili wapate ulicho nacho
Kuna watu wanasubiri ufe na wameshaanza kuchagua mashamba watakayorithi, wengine wamechangua ngíombe watakayochukua, wangine wamejichagulia mali zako
Kuna watu wanajiandaa kuoa mke wako ukifa
Wengine wamejiandaa kuolewa na mume wako
Wengi wap ni ndug uzako!
Wengi ni rafiki zako!
Waambie sijafa bado
Inawezekana nateseka, inawezekana niko kwenye matatizo lakini sijafa kiroho bado!
Nataka nimwabie Shetani leo, sijafa
Bado kuna muujiza unakuja kwa ajili ya maisha yangu!
Kwa ajili ya familia yangu!
Kwa ajili ya huduma yangu!
Inawezekana naugua
Inawezekana nimechanganyikiwa,
Lakini jambo moja unalotakiwa kulizingatia ni kwamba sijafa!
Makaburini ni mahali pa kumbukumbu
Ni mahali pa maombolezo
Na ndicho hasa kilichomfanya alien a kuomboleza kwa sababu aliwekwa mahali pa kumbukumbu na maombolezo
Makaburini ni mahali tunapotembelea lakini hatuishi makaburini na Yesu anakuja kumwokoa
Yesu amekuja leo kukuokoa usiishi kwenye mambo yaliyokufa, usiishi miongoni mwa waliokufa!
Ufunuo 3:8
Waebrania 9:14
Mambo tuliyoyazika, mambo tuliyopoteza, na shughuli ambazo hazikufanikiwa
Ni kawaida kukumbuka mambo ya nyuma inasaida kupata hekima ya maisha yajayo lakini ni jambo moja kukumbuka mabaya ya nyuma na jambo lingine kuchua mto na kwenda kulala kwenye mambo ya nyuma
Kuna watu hapa waishi kwenye makaburi ya hasara walizopata
Makaburi ya makosa yao na matatizo yao
Unapoanza kuishi makaburini ni ishara tosha ya kwa nini umepoa umekuwa vuguvugu na sio muda unakuwa baridi
Unajua kuwa kuna watu wanakwambia mambo uliyofanya miaka 20-30 iliyopita. Umevuka huko na bado wanahisi uko vilevile, wanaishi kwenye makaburi.
Ndio maana malaika alimwambia Mariamu usimtafute Yesu miongoni waliokufa
Luka 24:13
Kwa sababu ukikaa na makaburi kwa muda wa kutosha unakuwa kama rafiki zako
Yesu alitembelea kaburini lakini hakuishi kaburini anaishi mbinguni!
Waambie msinitafute makaburini, inawezekana nilikuwa makaburini uliponiona lakin unitarajie mimi kuishi makaburini
Ulikutana na mimi ijumaa, lakini leo sio ijumaa!
Nimefufuka na nguvu zote!
Naongea na wewe ulizimia,
Naongea na wewe uliyeanguka
Wewe uliyezimima kwa sababu ya vita ulizopigwa, umesinginziwa, umewekewa mitego na njama zikunase!
Waliokuchukia, Waliokukimbia!
Waambie ilikuwa ijumaa!
Usiishi walipokuacha
Usiishi walipokutupa
Usiishi walipokuuacha adui zako!
Wakikuona, waambie mlikosea! Njama hazikufanikiwa! Siwezi kufia hapa!
Mliniacha hapa lakini sitafia hapa!
Nilitembelea makaburini sitaishi makuburini!
Nikwambie jambo zuri? Waliokuacha makaburini utawaacha makaburini
Wewe utachapa kazi ya Bwana!
Bwana atakutuma ukahubiri, Bwana hatabaki makaburini
Waambie, nitatoka makaburini kwa gharama yoyote! Iwe kwa maombi, iwe kwa kuimba,iwe kwa kwa kuhubiri, nitatoka hapa maana hapafanani na nyumbani
Waambie Yesu aliyemwambie Zakayo mkuyu haufanani na nyumbani atanirudisha nyumbani
Kwa sababu mahali wamekuacha hapafanani na hatima yako. Walikuahidi kukusomesha
Walikuahidi kukuajiri
Walikuahidi vingi ili ubaki makaburini maana ahadi zao ni pingu
Ahadi zao ni minyororo!
Sitafia uliponikuta, sitafia uliponiacha
Usinifunge na ahadi zako, Usinifunge na minyororo matendo yangu ya zamani wakati matendo yako ya zamani husimulii.
Natoka!
Naondoka!
Nakuacha wewe makaburini. Uombleze juu ya nguruwe wako!
Uomboleze juu ya mapepo mliyonifunga nayo!
Natoka!
Natoka kwenye madeni, natoka kwenye umasikini, hata kwa kukjivuta natoka hata kwa gharama ya kujichovya Yordani
Umekuwa mpweke muda mrefu, Umetengwa muda mrefu
Umpweke umekutesa na kukuumiza. Kataa kufungiwa kwenye kabati, kata kufungiwa kwenye mafundisho manyonge
Usifungiwe makaburini!
Najua mnafurahia mimi kuishi hivi nilivyo, najua hampendi nikiishi kwa furaha, lakin natoka
Ninatoka hata kama mnaendelea kunisema, Semeni yote mnayoweza lakin nataka
Najua hamtasema nitakapoishi kwenye ahadi za Mungu, nitakapoishi kwenye ndoto zangu
Nitapambania njia yangu, naogopa lakin nitatoka, inawezekana natetemeka lakini natoka
Chochote ulichonifunga nacho navunja!
Umefika kwenye kongamano ambalo Mungu anakuita uingie kwenye upana wa uhubiri wako
Mungu anakuinua juu ya pito linalokukandamiza na ni wakati wa kuvunja
MAKABURINI:
1. Walimtupa makaburini
2. Yesu aliyafukuza mapepo makaburini-makaburi ni mashimo
3. Wenye nguruwe walimfukuza Yesu atoke
4. Yesu alimtoa aliyekuwa mapepo atoke Kaburini arudi nyumbani
5. Kaburini walibaki waliomtupa, Makaburini walibaki waliomfukuza Yesu, Kaburini watabaki waliopanga njama za kukuzika!
III. MINYORORO NA PINGU:
Pingu na minyororo walizomfunga nazo zilikuwa kwa ajili ya kumbakisha walipotaka afie
Ndio! Vyeo vingine wanavyokupa ni pingu na minyororo
Maneno ya watu dhidi yako ni pingu
Ahadi zao kwako ni pingu!
Zawadi zao ni pingu, uendelee kuishi makaburini. Toka!
Walikusemea manuizi tangu ukiwa mtoto yamekuwa pingu. Vunja
Wanakufunga kwenye minyororo ya mitazamo yao
Vunja, vunja!
Roho Mtakatifu amenituma kwako, niivunje minyororo, nivunje pingu
Navunja pingu alizokufunga baba yako, alizokufunga mama yako, walizokufunga ndugu zako, walizokufunga rafiki zako, walizokufunga viongozi wako navunja!
Tusi alilokutukana mwalimu shuleni lilikuwa pingu mpaka uachukia hesabu, ukachukia shule, ukachukia sayansi.
Vunja!
Kuna watu wamekuja kwenye kongamano na wengine wamekuja kuvunja pingu na minyororo-usiondoke kama ulivyokuja!
Kuwa muhibiri haimaanishi kwamba huwezi kuwa na maendeleo
Ukila nyama wanasema ni hela za kanisa-vunja hizo pingu
Ukinunua pikipiki wanasema ni hela za kanisa
Ukianzisha misheni watakwambia misheni gani haina mzungu-vunja pingu hizo
Ndio maana niko hapa kukwambia hata muhubiri anaweza kula nyama choma!
Kila pingu ina lengo la kukufanya mnyonge, inalenga kukufanya mpole ili uishi kwenye vipimo vyao
Vunja pingu!
Biblia inasema hakuna aliyeweza kumfunga! Angalau huyu alikuwa nafuu kuliko wengi wetu.
Mwambie jirani yako ìhuwezi kunifungaî
Sengenya sana, lakini huwezi kunifunga
Tukana sana lakini huwezi kunifunga
IV. MADHARA YA MAJERAHA YA PINGU:
Je Yule mtu alikubaliana na kufungwa?
Hapana!
Angekubaliana na pingu, asingeweza kumkimbilia Yesu
Ukikubali pingu hutafunguliwa
Nataka nione Kongamano hili likikufungua chumbani kwako, sebuleni, jikoni, na nataka kuona ukifunguliwa kanisani.
Kwa hiyo tumeona makaburi hadi minyororo na kutoka kwenye minyororo hadi kulia
KULIA MCHANA NA USIKU
Kila unapoishi miongoni mwa waliokufa unazuiwa na minyoro ambapo wengine wanafurahi kuzuiwa kwako
Watu watakufunga kwa faida ya furaha. Unasema mimi ni mtulivu na mpole kwa sababu naishi kwenye vipimo vyako
Kufungwa kwake ilikuwa ni utulivu wa ndugu zake na rafiki zake
Kufunguliwa ilikuwa ni usumbufu kwa ndugu zake,
Nawaza kama alikuwa na mke na watoto
Nawaza kama alikwa na wazazi
Jiepushe na watu wanaojifanya wanakujua sana!
Sisemi Yule mtu hakuwa na matatizo, na sisemi alikuwa na matatizo ila nasema alikuwa pia na ahadi
Na unapokuwa umenaswa kati ya matatizo yako na ahadi watu wanakufunga na kukutupa makaburini
Lakini kila walipomfunga alivunja minyoyoro. Walifunga nje wakati tatizo liko ndani, walifunga mwili wakati tatizo liko rohoni, Waliufunga mwili wakati tatizo haliko kwenye mwili
Yatazame maisha yako yalivyaa alama za minyororo watu walizojaribu kukufunga
Yatazame maisha yako ya nyuma uone walichokusemea watu kwamba hutafika mbali
Utaishia hapohapo. Wote walikosea! Mungu amekufungua
Sio lazima unipende lakini huwezi kunifunga
Hakuna awezaye kumfunga aliyefunguliwa na Mungu mhh,
5Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
Nataka niseme na wewe kuhusu nyakati za kulia
Sijui ulivyolelewa, lakini mimi nililelewa katika mazingira kwamba huruhusiwi kulia.
Kulia kunauma! Lakini hata kama kunauma nilitamani kulia ili nipate nafuu ya maumivu.
Majonzi hayaondoki kama machozi hayatoki. Kulia ni muhimu
Kulia hakukufanyi uwe na nguvu,kunakufanya uishiwe nguvu
Kama hujanielewa ni hivi; Kuna wakati maishani mwako inabidi ulie hata kama hujafiwa.
Inawezekana unalia kwa ajili ya nguvu kubwa uliyumia kufanya kazi ambayo hakuna anayekujali
Unalia kwa ajili ya muda ulioutumia kusaidia watu ambao leo wanakufunga pingu
Unalia jinsi ambavyo unatamani watu wajue unachojua lakin hawataki
Kuna mambo mengi ya kulilia unapoomboleza
Mume wako analia lakini anangoja ulale ndio analia
Mke wako anangoja ulale ndio analia
Kama unataka Mungu asikie, Lia!
Mtu asipolia anaweza kujinyonga
Kuna kilio kinaweza kumfikia Mungu1 Kilio kinakamata Mungu!
Kama huamini muulize Bartimayo,
Kadri walivyomnyamazisha ndivyo alizidi kulia
Alilia hadi Yesu alisimama. Kuna kilio ambacho kinashika Bwana, anasimama!
Waulize Waisraeli
Kilio chako kitamfanya Mungu asikilize na kuona kinachoendelea
Nikujulishe?
Kilio kilimfanya Yesu adhamirie kuvuka ngíambo.
Kilio chake kilmfanya Yesu avumilie upinzani baharini
Daudi anasema maskini Amelia na Mungu amesikia kilio chake, na kumwokoa
Kama utafungua kinywana kulia, Mungu angekuokoa
Tatizo sio Mungu, tatizo ni kwamba mdomo wako umeufunga, ukifungua mdomo wako, Mungu atakuja kukuokoa
Sishangai kuona upepo haukuzuia Yesu, Sishangai kuona mawimbi hayakumzuia Yesu. Ilikuwa ni lazima avuke ngíambo maana kulikuwa na kilio
Fungua mdomo!
Fungua mdomo
Tema, lisema
Sijali likoje lakini tema
Yesu atasimama kama utalia. Kilio kinamfikia Mungu!
Najau huamini, lakini muulize Habili, Damu ilipolia Mungu alizungumza akasema nimesikia kilio cha damu!
Unataka kujua damu nini? Damu ni uhai na uhai ni pumzi, Lia!
Walipotupa Yona, Alilia na Mungu alisikia
Hana alilia!
Lia Mungu atasikia.
Biblia inasema alilia mpaka akaoenekana kama mlevi kumbe amelewa maumivu, kumbe amelewa maombi
Ndugu yangu acha kuguna, Lia
Biblia inasema Yesu alilia
Kama Yesu anaweza kulia kila mtu anaweza kulia
Katika kitabu cha ufunuo Biblia inasema, nikasikia kilio cha roho zilizo chini ya madhabahu zikisema hata liniÖ.
Sema hata lini? X3
Mwambie Mungu imetosha!
Hutafia makaburini, Usifumbe mdomo
Biblia inasema;
5Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
Alilia makaburini na milimani, Bila kujali uko juu au uko chini Lia. Unaelewa kwa nini wengine wanalia wakiwa bondeni lakini ogopa watu wanaolia wakiwa mlimani
Ukiwa mlimani hakuna anayetarajia kukuona unalia
Wamezoea kuona walio bondeni kulia
Wasomi wanalila, Wenye vyeo wanalia
Kulia ni zawadi kutoka kwa Mungu
Usipokitapika kilicho ndani yako kitakutafuna, kitakupa kichefuchefu, Kitakupa presha, kitakupa sukari na vidonda vya tumbo
Acha kuweka siri
Lia
Usirudi nyumbani na hali uliyo nayo
.
KWANINI YULE MTU ALIMKIMBILIA YESU?
Ni lazima nikwambie kwanini yule mtu alimkimbilia Yesu
Hata kama alimkmbilia Yesu, mapepo bado yalikuwa yanaendelea kuongea
Safari hii yaliongea na anayemkimbilia
Alikuwa anakimbia, mapepo yalikuwa yanaongea
mapepo yalikuwa yanaongea lakini hayakuweza kumzuia kumkimbilia Yesu
Unatakiwa umkimbilie Yesu hata kama Iblisi bado anaongea kihwani mwako!
Sijali amekwambia nini, Sijali amemwambia nini Yesu kwa ajili yako
Ninachojua ni kwamba natakiwa kukimbia hata kama anaongea
Kuna watu wanataka kukusaidia, lakini adui ameenda kuongea naye wasikusaidie
Kuna watu wanataka kukusomesha, lakini adui amewambia huna tabia nzuri
Usikate tamaa! mkimbilie Yesu hata kama anaongea na Yesu
Wengine wameomba kwa Mungu uporomoke kiuchumi, mkimbilie Mungu tu
Nataka uelewe hili kwa sababu ni muhimu sana
Tumeona Mawimbi baharini, tumeona mateso ya kuishi makaburini, tumeona pingu na minyororo ya ndugu na marafiki, Tumeona kilio hadi kujikata kata mwenyewe
Sasa nataka nizungumzie kujikatakata
Biblia inasema alikuwa najikatakata mwili wake mwenyewe
Kila kitu kilichotokea nyuma kilitokana na watu wengine
Walimfunga minyororo na pingu lakini alizikata-Kumbuka tumesema pingu ni manuizi, lawama, mashitaka na maneno ya maadui kwamba usiende popote
Walimtupa makaburini
Lakini alipokuwa peke yake, alijikatakata
Sasa nazama, nazama hapa kwenye kujikata
Nataka uyafahamu madhara uliyojifanyia mwenyewe, Mambo ulijiumiza mwenyewe baada ya kutupwa, baada ya kusahauliwa
Baada ya kukimbiwa! Baada ya kusalitiwa!
Tazama hili;
Huyu mtu yuko makaburini, ana marafiki ambao hawezi kuwafikia
Ana ndugu na wazazi ambao hawezi kuwafikia
Ana watu aliowahi kuwasaidia
Lakini yuko makaburini.
Ana maisha mambayo hawezi kuyafikia
Ana kitanda lakini hawezi kulalia,
Ana nyumba labda
Unapotoka kutendewa mabaya na watu ambao ilikuwa wakutendee mema kwa jinsi ulivyowajali,
Unapotoka kusemwa vibaya na watu ambao hata hawasemi ukweli,
Kwa kuwa huwezi kushindana nao, kinachofuata ni lazima ujifunze kushindana moyo wako ili ushinde.
Linalofuata unaanza kuchukia uliyotendewa badala ya kumchukia aliyekutendea
Hatua hiyo inakuingiza kwenye kujidhuru
Kila kitu na watu wanaokuzunguka kinapokugeuka
Hasira yake ilirudi ndani yake kumtafuna!
Hiyo inaitwa msongo wa mawazo
Msongo ni hasira iliyotumbukia ndani
Hasira usipoitoa nje inarudi ndani
Ikitumbukia ndani inakufanya ujikate mwenyewe
Itakufanya uwe adui yako mwenyewe!
Mungu nihurumie, najisikia kuhubiri..
Itakufanya ujiue,
Biblia inasema, wakati yuko peke yake alikuwa najikata mwili mzima
Kwa nini ajikate!
Inaitwa dawa ya maumizi-maumivu kwa maumivu
Umesalitiwa unajinyonga!
Umedhulumiwa unajua!
Kudhulumiwa ni maumivu na kujiua ni maumivu!
Maumivu kwa maumivu ni pale watu wanapojaribu kutibu maumimvu ya ndani kwa kujiumiza kwa nje
Wanaokutukana wanakuumiza kwa ndani, maumivu yao hayatoki damu lakini wewe unajiumiza kwa vidonda vya tumbo
Wanaokusaliti wanakuumiza kwa ndani lakini wewe unajinyonga
Ukweli ni kwamba kujikatakata hakukuondoa maumivu ya moyo.
Haijalishi unakata kimwili au kiakili unafanya hivyo ili kuepuka maumivu uliyo nayo
Unazima moto kwa kutumia moto
Hii ni tabia ya kujiua
Ungeweza kuitoa hasira kabla haijakimbilia ndani
Ungefanikiwa kimaisha lakini unajikata
Ungeheshimiwa lakini umejikata, unajiona huna faida
Umekataa kufanikiwa kwa sababu umekubali kujiumiza
Kila wakati ukionewa huli chakula, huendi shambani, unashinda umeinama. Unajikata
Unajiona huna maana, kwa sababu wamekuona huna maana
Kinamfanya adui akufanyie hivyo ni kwa sababu anataka ujiue mwenyewe bila yeye kukuua
Kataa kufa!
Kila wakati unapata nafasi ya kupanda juu lakini unajiona huna lolote
Lakini, mashua ilipofika ufukweni…..
Habari ilibadilika!
Mashua imefika leo, imekufikia
usiondoke kama ulivyokuja
Mashua ilipofika, alimkimbilia Yesu,
Mapepo 6000 yako ndani ya huyu mtu hayakumzuia kumkimbilia Yesu
Kama uko tayari kumkimbilia Yesu hakuna litakalokuzuia
Mapepo hayakuwa na uwezo wa kujificha tena, hivyo kabla hajaongea yaliongea yenyewe
7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. 10Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
Mapepo yalijua Yesu ni roho na yenyewe ni roho
Yakobo 2:19
MAshetani yanaamini na kutetemeka
Kama huamini waulize wana wa Skewa.
MAPEPO YANA MIPAKA YA UTAWALA:
Mengine ni ya familia, mengine ni ya kijiji, mengine ni ya wilaya, mkoa Taifa, ukanda, Bara na dunia
Nakwenda kinyuma na mapepo ya mkoa wenu yanayotawala eneo la maisha yako
Kuna eneo lina nafsi shetani anataka kulikalia kwenye Kanisa-
Na hataki kuondoka kwenye hili eneo mpaka amalize muda wa malengo. Mpaka akuharibu kabisa, Mpaka akuue kabisa, Mpaka ufukiwe kaburini
Aliingina kwenye ukoo muda mrefu ndio maana sehemu hatari kukaa ni misibani!
Muda wangu hautoshi kukufundisha msiba na mapepo. Mapepop hayana mwili na yanahitaji mwili ili kufanya kazi yao
Hayawezi kufanya kazi hewani yanahitaji mwili wa kufanyia kazi
Na yakasema, kama unatutoa tunaomba tuwaingine nguruwe!
Inawezekana kulikuwana mabishano kabla ya kufikia uamuzi wa kuwaingina nguruwe
Unajiuliza najuaje, najua kwa sababu biblia ni ramani, sio nyumba ya kuishi. Yameandikwa tu yale ya kutufikisha tunakokwenda
Kwa hiyo Jeshi moja la mapepo lililokuwa kwa mtu mmoja,
Oh mtu mmoja!
ìKushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu yaÖÖ.majeshi ya pepo wabayaî
Yule aliishi na jeshi la mapepo ambapo nguruwe 2000 hawakuweza kuishi nao hata kwa dakika moja
Nguruwe walipoingiwa na mapepo yaliyokuwa kwa mtu mmoja, nguruwe walijiua
Nguruwe waliojiua, mapepo yalikosa pa kukaa na yako kwenye maji
Kumbuka pepo amtokapo mtu hutafuta mahali pasipo na maji
Nguruwe walisema,
Nguruwe walisema, ni heri kuzama kwenye maji kuliko kuishi na mapepo
Nami nakwambia nakwambia ni heri kubatizwa kuliko kuishi na mapepo
Ndio maana ubatizo ni muhimu, kwa sababu sio tu unaondoa dhambi lakin pia unamzamisha shetani, unayazamisha mapepo
Ndio maana Yesu mpaka leo analisafisha kanisa kwa neno na kwa maji.
Kanisa, nimesema Kanisa.
Nguruwe wanaona ni heri kufa kuliko na hali ambayo kanisa linaishi nayo.
Umekuwa ukipambana na mambo ambayo ni magumu kiasi cha kukuua
Nayatangazia mapepo leo, mwili wako sio hekalu lao
Sijui utaenda wapi baada ya kutoka maburini lakini najua utakuondoka hapa tofauti na vile ulivyokuja
Simama mfukuze shetani mbele yako!
ì Wala msimpe shetani nafasiî
Jifunike na damu ya Yesu, Jifunike na ubatizo, kila napotaka kurudi akute sio wewe ni Yesu
ìwaliobatizwa katika Kristo wamemvaa Kristoî
Tangu sasa mtu asinitaabisheÖî
Yachanganye mapepo, yape msongo wa mawazo, yatoke yakidhani yatakuwa hai kmbe yanaenda kuangamia
Sio lazima moto uyaunguze, hata maji ni sumu yao
Hata maji ni kaburi lao.
Tumia siku ya leo kuachana nayo. Unalala nayo, unakula nayo yazamishe baharini
Swala si yanaenda wapi bali ni kwamba yalipo si mahali pao!
Mapepo yakatumbukia majiniÖ
JAMBO LA MWISHO:
Mapepo yanatafute mahali pasipo na maji, yazamishe kwenye maji
Aliyekuwa anajkatakata makaburini, Yesu alipomaliza tatizo lake, alirudiwa na fahamu zake
Ndugu zake hawakufurahi ndio hofu yake,
Hakujua mapepo yamezamishwa, ndio iliyokuwa hofu yake
Aliogopa kurudi nyumbani, nyumbani ndiko yalikomwanzia
ìNataka niende na weweî na anamwambia nina kazi na wewe huku Dekapoli
Kwa mwonekano wa nje kuna furaha lakini upande wa pili kuna hofu ya kurudi nyumbani
Jambo lililomzuia kwenda nyumbani lilikuwa ni kuwa nyumbani
Hahahaha, kuwa nyumbani kunatisha, kunaleta hofu
Nyumbani ndiko kunakupiga vita, nyumbani wanakuwana amani ukifeli.
Nyumbani. Yesu akamwambia rudi nyumbani.
Tukiwa kwa watu tunacheka, watu wanadhani tuna furaha lakini tunaogopa nyumbani.
Jambo gumu kwa mwanaume ni kurudi nyumbani
Hata kama akienda kimwiliÖwanagapi tuko nyumbani, wangapi tuko hapa!
Kwenda nyumbani ambako hujaenda nyumbani ndiko kunasababisha wanaume wengi wakifika wanazunguka nyumba kwanza, wanaenda chumbani ndippo wanakuja sebuleni kwa sababu wanaiona nyumba kama kazi mpya.
Yesu akamwambia nenda nyumbani ili uwe nyumbani, nyumbani ni kuzuri lakin ni gharama kuwa nyumbani
ìAdui za mtu ni wale wa nyumbani mwake mwenyeweî
Yesu alivumilia vita ya baharini kabla hajamkomboa Yule mtu na hakutaka aondoke naye.
Hata kama wamemkataa Yesu, hata kama wamemfukuza Yesu, Yesu anataka Yule mtu akawe mahubiri ya kila siku kwao
Akachukue nafasi iliyokaliwa
Hahitaji kuandika kitabu wala kuandika Biblia bali akae kibalazani akinywa chai
Ni mahubiri tosha
Amani yako ya ni kitisho tosha bila Yesu mwenyewe
Umekuwa ukiwaza kwa nini unapanda lakini huvuni kama ulivyopanda
Umekuwa unawaza kwanini unatoa lakini hufanikiwa
Ni kwa sababu Mungu amekuwa akipeleka Baraka nyumbani kwako lakini uko makaburini umebadilishana Baraka na makaburi
Ukiwa nyumbani, nyumbani hasa ambako hujikati unaiona thamani yako, huwazi kujiiua kwa kushindwa
Ubunifu wako unakuwa juu
Mafanikio yanaongezeka
Amani inapoongezeka, nguvu inaongezeka!
Vile unapojikuta ukilala hujui kama funguo za chumbani zitakuwepo ili utoke au mtagombana hadi ushindwe kutoka
Unapoona unawaza kurudi nyumbani lakin unatamani ukute wamelala na hujui kama watakufungulia-huwezi kuwa nguvu, leo rudi nyumbani ukahubiri mambo aliyokufanyia Yesu!
Mafanikio yako, amani yako, nguvu yako vinahitaji uwepo wako lakini umekuwa ukiishi makaburini
Mtu Yule alitaka kuodnoka na Yesu, hakujua kama Yesu ametangulia nyumbani na anamsubiri yeye
Unaporudi nyumbani, Yesu ametangulia. Unajiuliza kivipi.
ZAkayo aliambiwa wokovu umefika nyumbani mwake wakati yuko juu ya mti
Yesu alimwambia pepo akahubiri, ìnami niko pamoja nayi hata ukamilifu wa dahariî
Sio kwamba Mungu hakupendi ila wewe ndio hujipendi. Watu wasiojipenda hudhani hawapendi
Watu wasiojiamini huwawamini wengine
Wasiojipenda ndio wasiopenda na wasiojiamini ndio ambao hawawaamini wengine
Mungu anataka urudi nyumbani, ukae nyumbani na wewe mwenyewe
Acha kujumiza kwa ajili ya mambo ambayo huwezi kuyadilisha, rudi nyumbani. Yaliyotokea huwezi kuyabadilisha. Yaliyopita yako makaburini usiende kuishi kuishi makaburini.
Rudi nyumbani!
Acha kuishi na waliokufa
Makaburi tunayatembelea hatuishi, makaburi sio nyumbani. Hakuna hoteli makaburini
Jambo moja ninalijua kwa hakika ni kwamba hutaondoka kama ulivyokuja.
Utaondoka umenichukia
Utaondoka ukiwa umefukuza hahahaha
Kwa sababu nimekuzamisha majini ulipodhani utaishi kwenye nguruwe kwa muda ili umrudie tena aliyepona
Usiondoke kabla hujabadilika.
Kwa nini unawaza kujiumiza, Mungu anajua, Anajua
Ndio maana;
ìKwamaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kilaÖî
Mungu anakuppenda na hakuna anayekupenda kama Mungu-Kafanye kazi yake
Hakuna anayeweza kuchukuliana na wewe kama Mungu
Ukiwa uchi usiogope, Mungu anakujua
Mungu akubariki, awabariki wanao na binti zako
Natamka kuongezeka kwako
Natangaza mafanikio katika maisha yako. Sio utajiri tu bali hekima na ujasiri na nguvu na kuridhika
Umetoka mbali
Kwa nini uendelee kuishi na uchungu na hasira
Lolote linalokutesa na kukupeleka makabirini achana nalo leo. Rudishamani yako
Acha kuhangaika kuweka viraka kwenye mioyo iliyokukimbia, mioyo iliyokutupa
Mioyo iliyokuchukia
Pata amani, keti kibalazani wakuone. Waambie sijafa
Usihangaike kubadilisha akili zao.
Mungu ameniambia nikwambie USIONDOKE KAMA ULIVYOKUJA!
Sasa nyosha mikono juu shetani ajue hujafa!
Tuombe.