All Sermons
Bible Passage Marko 16:15
This content is part of a series Mahubiri, in .

UONGOZI NA UINJILISTI

Date preached May 18, 2025

Marko 16:15

UTANGULIZI:

* Nataka uone jinsi somo hili linavyoweza kukupa fikra na mawazo yatakayokusaidia kutambua ulipo.

 

* Nitakuwa naelezea jinsi ya kujenga ulipo kwa kuwaza mbali

 

* Kwa ajili hiyo, nitatumia “Enendeni ulimwenguni mwote” kama “enendeni mbali”

 

 

 

Enendeni mbali:

Kuna msemom usemao “gharama ya kulea mtoto ni kijiji”

-Wazazi hawawezi kufanya/ kulioa gharama zote za kulea mtoto bali inagharimu jamii nzima kumwendeleza na kumkuza mtoto.

 

Gharama ya kulea mtoto ni kijiji.

 

Kama ambavyo inagharimu kijiji kulea mtoto, ghrama ya kulea kanisa ni kijiji.

 

Kijiji nini? Seth Godwin katika kitabu chake cha ushawishi na mvuto anasema kijiji ni;

* Ni makabila

* Vikundi

Facebook, twitter na instagram inaita wafuasi

 

Mahitaji ya Uongozi;

Uongozi unahitajika, lakini uongozi unahitaji nini?

 

Uongozi ni ushawishi katika mzunguko (circle) ambao uko ndani yake.

 

Wengine huridhika na ushawishi walionao kwenye kijiji

 

Ukweli ni kwamba hii ni kwa sababu kilichokulea kinaweza kukugeuka na kukudumaza

Kukuzuia.

 

Katika somo hili nitaangazia ubaya wa kijiji kwa mtumishi anayetaka kuwa kiongozi.

* Si kila mtumishi ni kongozi

 

Ukiangalia katika Matendo 8 utaona kwamba Yerusalemu iliyolea kanisa ikawa kizuizi cha Kanisa kuenea

 

-Yerusalemu ni kijiji kwa mujibu wa somo hili

* Mahali palipozoeleka hata kama kuna akina Anania na Safira

* Ni mahali palipofanyika vikao vya kanisa

 

 

 

Mfumo wa jamii ni watu wachache wanaokupa kuridhika kwamba tayari uko mbali

 

Katika kijiji unatulia

Katika kijiji mambo yanaenda vizuri

Katika kijiji kila unachosema wanaitikia Amina

 

KIsha unamwambea mtu anayeenda mbali wakati uko kijiji kwa sababu unadhani anapata mapingamizi na vita nyingi kuliko wewe.

 

Ni vile tu uko kwenye kijiji ndio maana huna vita na vita uliyonayo ni kiwango cha kijiji kwa sababu umeridhika kuishi kwenye kijiji.

 

Nataka nikwambie leo kwamba kwa kadri unaendelea kuishi kwenye kijiji, kwenye duara lako hakuna vita wala vikwazo

 

Kama Mungu;

* Atakuinua kupita ya duara ya kijiji

* Akakuondoa kwenye duara ya Kijiji,

* Akikutoa kwenye mazingira uliyozoea (mazingira ya makuzi, mazingira ya kitheolojia, mazingira ya kihuduma)

 

Bado hujadaka ninachotaka kumaanisha, umedaka tu nilichosema;

Ni hivi;

Kama Mungu;

* Angekuweka kwenye vipenyo vingine kwenye bwawa la fikra ambako hakuna anayekubaliana na kila Haleluya Ni kwa sababu Mungu angekuwa anataka ukue kiuongozi

* Ambako Yesu ni Bwana kwenye utata

* Ambako kilichokuwa Amina kwenye kijiji chako kwenye bwawa la Fikra linashambuliwa

 

Una nguvu za kutosha kutotamani masufuria ya nyama, mikate na matango uliyokula kijijini

 

Hutakubuka vitunguu swaumu vya Misri?

 

Je hutasema narudi kule nilikozoea?

 

Hakuna misheni nyepesi kama iliyo na wazungu hata kama watoto wangu wana lala na njaa, hata kama Ukristo wangu unakufa

 

Je, una ubavu wa kutosha kuingia kwenye bwawa ili uende mbali?

Je una hofu ya kukosa ameni ya wanadamu na hivyo uko tayari kufia kihuduma kijijini kwenu?kwa sababu unahitaji waridhie ndio ujisikie vizuri

 

Je ni ridhaa ya kijiji chako ndicho kimekukwamisha kuwa kiongozi unatakiwa na umegeuzwa na kijiji kuwa yaya, mlea watoto. Unalea na kutumikia fikra za kijiji hata kama kukubalina

 

 

Nimezaliwa na kukua kwenye kijiji, na sijawahi kuondoka kijijini. Kadri nilivyoendelea kuishi mambo yote yalikuwa mazuri.

 

Nilikitetea kijiji katika kiwango cha kukwasaliti hata rafiki zangu waliponishauri kuwa nje ya kijiji kuzuri zaidi

 

Wakuu wa kijiji waliniweka kama mpelezi wa kijiji. Niliwachukia wote walikisema vibaya kijiji kwa asababu kwenye kijiji kuna kila kitu nilichohitaji

 

Ukiishi kwenye kijiji unaishi kwenye banda

 

Kuna watu wanaishi Rukwa hawajawahi kwenda Mbeya ambako hawaju Posuta na wanaojua Posuta hawajui Koyi na wengine hawajui Msindile

 

Ni kwa sababu tumekizoea kijiji chetu nap engine tumejenga sana kwenye kijiji. Labda ni vizuri kwa sababu hutaki kuwa kama viongoz ambao wanajenga ulimwenguni wakati kijiji kinabomoka.

 

Sio kwa sababu unajenga katika kijiji ndio usiwaze nje ya box la kijiji. Usipojitahidi kuwaza nje, kijiji kitaota miiba kukulazimisha kuondoka kwenye utulivu wako ili uende kwenye shabaha yako.

 

Naeleweka?

 

Wakati mwingine kuzimu inafunguka ili utoke kwenye kijij

 

Namaanisha hivi;

* Wakati Fulani tai huweka miiba kwenye kiota ili makinda yasitulie mahali walipozoea ili yaruke juu

 

Huo ulikuwa ni utangulizi:

 

Hongera ziwaendee wawili watatu waliodaka utangulizi;

 

TOKA NJE YA HEMA UONE MBALI

 

* Jambo lingine baya ni kuwa mhubiri bila kuwa kiongoziInabidi Lutu aondoke maishani mwako ndipo Mungu aongee na wewe

 

15Nchi hii yote unayoiona nitakupa wewe na wazawa wako iwe yenu milele.

16Wazawa wako nitawafanya wawe wengi wasiohesabika, kama vile mavumbi ya nchi yasivyoweza kuhesabika!

* Kutokuwa na mtoto kulimfanya Ibrahimu asipende kuachana na Lutu

* Kutoachana na Lutu kulimfanya Ibrahimu asionyeshwe nchi yote

* Unaye Lutu kijijini ndio maana huwezi kuona mbali

 

17Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.” 18Kwa hiyo, Abramu akangoa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.

* Hakwenda ili akaipokee ahadi, bali akaitembelee kwanza

* Inuka utoke!

Inawezekana umeridhika kwenye hema lakini Mungu hajaridhika na wewe kuongoza ndani ya hema

 

Mungu anataka uangalie Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi

 

Inuka, utoke!

Kuinuka ni kazi

Kutoka ni kazi!

Lakini huwezi kuwenda Mashariki, Magharibi, kusini, Kaskazini kama huwezi kufanya kazi hizo mbili

 

Sijui mengine aliyokusudia Mungu kwako ambayo bado hujapokea kwa sababu tu uko kwenye hema, uko kwenye kijiji, uko kwenye banda.

 

Ukiwa kwenye banda, ukiwa kwenye hema, ukiwa kwenye kijiji sina uhakika unaona umbali gali gani zadi ya kuta za banda, zaidi ya kuta za hema

 

Kuna ulimwengu nje ya hema

Kuna ulimwengu ya Banda

 

Ndio maana sijui ni kiasi gani unajua kumhukumu mtu aliye katika mipaka ya ulimwnengu wakati upo kwenye mipaka ya kijiji.

 

Kuna ulimwengu nje ya kijiji

 

Mathayo 28:18-20

Matendo 1:8

Mungu alisema “uinuka, ukaitembelee nchi nitakayokupa.” Kisha Ibrahimu –AKAINUKA,

Anapoinuka akang’oa hema. Akang’oa hema, AKAING’OA HEMA.

 

Kabla semina hii haijaisha utang’oa hema,

Kabla semina hii haijaisha utang’oa banda ili uende Mamre na huko utamjengea madhabahu Bwana

 

Aya hii inatwambia hema (iliyokuwa inajengwa kama duara, msonge au mzunguko) na ina wito wa ulio duara, mzunguko (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi.

 

Aya hii inatonyesha jinsi mawazo ya Ibrahimu yalivyokuwa kwenye kingo za duara ya hema

 

Ayah ii inatwambia jinsi mawazo ya Ibrahimu yalivyotakiwa kuwa kwenye duara ya kingo za ulimwengu

 

Haleluya!!!

Hizo ni sababu mbili kwanini nichagua aya hii kama fungu la kutoka kwenye kijiji ili uende ulimwenguni mwote Marko 16:15

 

* Alipokuwepo Ibrahim, Alipo Ibrahim na alikokuwa anaenda.

* Alikuwa Misri (Mila na utamaduni na Mali),

* Alipokuwepo (mahali panapofaa kwa mifugo na alipazoea)lakini ni kijiji

* Alikokuwa anaenda (Ulimwenguni, asikokuzoea)

 

Mungu hutupeleka tusikokuzoea ili tukahubiri imani baada kutupima imani

 

Ulipoketi asubuhi hapa umeketi na mambo matatu lakini nina uhakika utaondoka na moja au utaondoka nayo matatu.

 

Ulipokuwa, ulipo na unakokwenda yote matatu umekaa nayo, unatembea nayo. Kwa sasa unakaa nayo kwenye kiti. Hata unapokula

 

Haiepukiki

 

Sisi wanadamu hatuwezi kukuelewa jinsi unavyowaza, au jinsi unavyoongoza au unavyoendesha mambo tusipojua ulikotoka. Kwa sababu kuna uhusiano kati ya ulipo na ulikotoka.

 

Na huwezi kutumika na Mungu kama hujui ulipo sasa.

 

Adamu uko wapi? Sio Adamu ulikuwa wapi na sio Adamu unaelekea wapi

 

Huwezi kusonga mbele kama hujui uko mahali gani. Huwezi kuona (maono) utakakokuwa usipojua ulipo

 

Hivyo;

Kwenye kiti ulichokalia ndipo ulipokuwa, ulipo na unakoelekea.

 

Nilipokuwa naondoka Lusaka kuja sumbawanga niliambiwa “sahau yote unayojua kuhusu kuhubiri mikutano ya hadhara uliyofanya Lusaka kwa sababu kule sio huku”

* Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo Wafil. 3:8;

* Kama kuna kitu kwenye maisha yako bado kina thamani, zaidi ya thamani ya ipitayo kiasi ya kumjua Kristo, kujua neno na sio kujua biblia, wito wa kwenda ulimwenguni mwote unaweza kupoteza wokovu wako japo unaendelea kusali na kuhubiri

* Sahau kule ili uende kule

 

Nilipoambiwa nisahau sikuelewa maana haikuwa kusahahu mji, watu bali ilikuwa ni kusahahu mtindo wa kufanya uinjilisti

Mtindo ndio unaoamua matokeo maana ni mchoro ndio unaopelea kuwepo gauni, kuwepo nyumba, mchoro

 

 

Utatumia mchoro wa nguo ambayo ulishona ukiwa na miaka 6 na sasa una miaka 40?

 

Kadharika mshono wa nguo ya wahuni huwezi kuutumia unapotaka kuondoka kwenye uhuni na ulaghai

Unaelewa?

 

Huwezi kuuingiza ulimwengu ndani ya kijiji chako bali kijiji chako unaweza kukiingiza kwenye ulimwengu.

 

Unajaribu kutekeleza wito wa kiulimwengu kwenye kijiji?

 

Unakuja kwenye Kongamano kama hili ili upate kipande hiki na kile ili urudi ukandike kwenye ukuta wa kijiji chako wakati hujaondoa kuta kichwani mwako

 

Umezipamba kuta zako kwa haya mafundisho,unatumia haya mafundisho kupaka rangi kuta za hema?

 

Hiyo ni ishara kwamba umekwama ulipo. Huwezi kung’oa hema hivyo huwezi kuona Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi

 

Hung’oi hema zaidi ya kuipamba kwa sababu unataka ukienda Mamre uwe unaweza kurudi kwenye kijiji

 

Nipe kichwa chako niseme nacho!

 

SIpo hapa kuwafurahisha. Hatujaitisha kongamano hili ili watumishi warudi kwenye kijiji

 

Kila anayejaribu kunitoa kwenye kijiji niliwahi kupambana naye.

 

Sitarajii kuona tabasamu lakini lazima tuchague kuwa kwenye kijiji (na kongamano litakuwa halijakusaidia) au tutoke tuone Kasikazini, Kusini, Mashariki na Magharibi

 

Najua, najua kuondoka kimwili kunauma lakini nakualika uondoke kifkra, kiroho itakuuma zaidi maana utalazimika kuondoka na kimwili

 

Kuna uwezekano mkubwa ukawa muhubiri bora sana lakini ukawa siyo kiongozi nasema tena. Kama kuhubiri kwetu kunapelekea makanisa kuanzishwa je nani ataongoza

 

Lakini pia unaweza kuwa kiongozi bora lakini sio muhubiri bora lakini unaweza kualika muhubir kuja kuhubiri unapoongozi kuliko unavyoweza kumwalika kiongozi kuja kuongoza

 

Uongozi unawapeleka watu mbele. Uongozi unaongea kwa kufanya. Uongozi unatumika kwa kutumika

 

Uongozi: nifuateni kuna mahali lazima tufike pamoja

 

Jambo baya ulimwenguni ni kukwama nyuma mtu ambaye hasongi mbele. Hawa ni watu tunakuwa nyuma yao tunapotaka kwenda wakati wao wamefika kwenye vyeo, kwenye maslahi.

 

Ukweli ni kwamba kama unataka kwenda mbele vyeo na maslahi na marupu rupu vinakudanganya kwa sababu unawezaje kuniongozi wakati uko kwenye hema miaka 20 sasa?

Mwambie jirani “songa mbele”

 

 

Jambo lingine baya ni kuwa mhubiri bila kuwa kiongozi

 

Mahubiri huvuta watu lakini kama hutawaongoza wataondoka

* Unaongoza au unahubiri?

* Unatambua vipawa vya unawaongoza

 

Utabaki na uchungu maana hujui kwanini wameondoka na hivyo utaendelea kuhubiri zaid na zaidi hadi mwishoni utakata tama.

 

Hawaondoki kwa sababu huwezi kuhubiri bali kwasababu huwezi kuongoza. Kila kundi linahitaji sio linatakiwa ila linataka kusonga mbele

Tuone kanisa lina mashule, lina vyuo vikuu, lina vijana kwenye serikali, Kanisa linakuwa na miradi

 

Hakuna anayetaka kuwa na kiongozi ambaye hasongi mbele lakini wengi wanataka kuongoza kundi linalosonga mbele.

 

Watu wanaamini katika kusonga mbele hawatakaa nyumba kiongozi ambaye hasonge mbele, amekwama. Hata familia hivyo hivyo. Familia ikikwama ni kiongozi amekwama, kiongozi wa familia akikwama wa nyuma watachukua usukani au watamkimbia hata kama ataishi nao.

 

Kiongozi aliyekwama nyuma yake wanakuwepo wale wasio na matunda. Watu wanaokuja kanisani wanapotaka. Wanaokula mkate na kunywa divai tu. Lakini wale ambao wanaamini katika maendeleo wataondoka.

 

Tunapima uongozi kwa kuangalia mabadiliko ya walio nyuma yako

 

Kama huendi mbele, unakuweje kiongozi?

 

Huwi kiongozi kwa sababu umesoma chuo cha Biblia, unakuwa kiongozi kwa sababu unajua neno la Mungu.

 

Uongozi hauvaliwi kama nguo za kanisani. Tumekuwa bango.

 

Kanisa linahitaji Sekta zote zisonge mbele

 

KUNA MAMBO MUNGU ANAGOJA LUTU AONDOKE NDIPO AKUONYESHE

Sio bahati mbaya kuona Biblia inasema,

 

“Baada ya kuondoka Lutu Mungu aliongea na Ibramu” Mwanzo 13:14

 

Kuna mambo ambayo Mungu hawezi kukwambia mbele ya Lutu hadi utakapokuwa kiasi cha kuweza kuwa tayarikumwondoa Lutu-Hadi uatakapoweza kumsikiliza Mungu kwa sababu Lutu ni neno ya ulikotoka.

 

Kwa ajili ya kongamano letu, Lutu ni itikadi, mtindo na mfumo uliotoka nao ulikokuwa

 

Kwa sababu umemzoea umemzoea, Lutu ni usingizi wa huduma yako

 

Kinachokukwamisha kwenda mbele ni watu uliowazoea na historia yako na Mungu hawezi kukuonyesha mbali mbele ya Historia yako na mbele ya watu uliowazoea

 

Unajuliza kwa nini?

 

Ni kwa sababu mtu hufanana na histroria yake na anaoshinda nao

 

Kwa upande mwingine Lutu ana maslahi na wewe ndio maana yuko na wewe. Lutu akiwa na wewe anajisikia vizuri sana

 

Kama hilo ndilo lililopo unatakiwa kuchagua, upenda kesho yako zaidi ya u navyompenda Lutu? Au inabidi ubaki kwenye kijiji. Kijiji ni watu na watu ni wale ambao wako kwenye simu yako.

 

Ukinipa simu yako nitakuonyesha kijiji chako. Hiyo ni nja nyepesi ya kufafanua maana kijiji

 

Kijiji chako kipo kwenye simu yako

* Watu wanaokupata

* Watu unaoongea nao

* Watu wanaotawala jinsi unavyotakiwa kuhubiri

* Watu unaowaambia shida zako

* Wanaowaza kama wewe

* Watu wenye mtizamo kama wewe

Hao ndio hema yako,hao ndio Lutu wako

 

Lutu alipoondoka, Mungu alitokea!

 

Ilikuwa ni vigumu kwa Ibrahim kumwachia Lutu aondoke, kipindi Lutu amezoeleka. Kitu gani kinasabisha ugumu wa wewe kumsikia Mungu?

 

Simaanishi kusoma neno la Mungu, wala kusoma Biblia. Nazungumzia neno lililo hai linaloweza kukujia mara moja, mara mbili au mara tatu maishani mwako

 

Linalobadili kabisa mwelekeo wako na kusudi kwa miaka kumi au ishirini ya maisha yako

 

Kama uko hapa na unataka kumsikia Mungu unatakiwa utoke kwenye parking ya magari uendeshe gari ukutane na trafiki kwenye barabara kuu. Ukutane na milima, na miteremko, na honi hadi unaishiwa mafuta

 

Ni lazima uondokane na watu wanaowaza kama wewe, Wanaosimamia hata mahubiri yako, lazima uende barabara kuu ambako kuna upinzani na vikwazo ili ufikie hatima yako.

 

Nakuhakikishia, jambo moja nililojua kuhusu wewe ni kwamba usingekuja kwenye kongamano kama Mungu hana ambacho hukuwa nacho kwenye parking. Mungu ana la kufanya na wewe

 

LUTU AKIONDOKA MUNGU ATAONGEA

Utulivu uliokuwa nao kwenye parking ni sauti zilizotaka ubaki kwenye kijiji na zinakuzuia kuwa kiongozi

 

Nataka kukwambia kwamba huu ni wakati wa kuvunja mstari, kuvunja kuta, kuvunja kikundi, kuvua cheo, uwe nje ya mazoea, nje ya kawaida. Watu uliowazoea hata hawajui kama unapumua.

 

Lakini huwezi kutoka kwenye maegesho kama unaogopa polisi wa barabarani. Tatizo tulilo nalo ni kwamba kwenye makanisa kuna watu wamejenga ufalme mdogomdogo. Ndio ukiwa unafundisha hawatasema amen mpaka wamwangalie mfalme wao akitikisa kichwa wanajua amekubaliana hawana ujasiri wa kutumia hata nywele zao wenyewe. Wanadhibitiwa na Mahitila wadogo. Akina Hitila uliowapa cheo cha kutawala huduma yako na roho yako na huna uwezo kuwaondoa maana umewazoea. Wamejenga minara hadi kwenye familia yako nikama kila unachopanga wanasikia.

 

Wanachofanya hawa makaisari ni kutoa unabii wakiwa kwenye choo cha kanisa huku wewe unashinda unapambana na ugomvi kwenye kanisa.

 

JIpige kifuani jiambie “Lutu akiondoka Mungu atasema name”

 

Jiepushe na Lutu, Jiepushe na Lutu. Najua umemzoea Lutu, Najua Lutu alikuletea mkate wakati unaanza Kanisa. Najua Lutu alikuletea blanketi mke wako alipojifungua. Najua Lutu ndiye anayekufikirisha unawaza kijiji. Lakini Lutu amekuwa mnara kwenye huduma yako. Unatakiwa uwe mwanamume kweli kweli, inabid uwe mwanamke vya kutosha maana Lutu akiondoka,

 

Lutu akiondoka, Mungu ataongea

 

Huu ni utabiri, Hii ni ahadi, huu ni uhakika! Lutu akiondoka Mungu atasema nawe!

 

Fikiria Ibrahim hakuwa amesikia sauti ya Mungu kwa miaka mingapi, wakati huu Mungu ataongea naye. Sijui kwanini sijamsikia Mungu muda mrefu hivi. Sijui hujamsikia Mungu kwa muda gani. Mimi nimekuwa naisubiria sauti ya Mungu.

 

Tatizo sio Mungu kuongea. Tatizo liko na Lutu.

 

Usichokiua, kitakuua

 

MUNGU ALIPOMTOKEA IBRAHIMU

Allipomtokea Ibrahim alimwandaa kuwa kiongozi

 

Kwanza alimwambia “Tazama nje”

 

Maono

Tazama nje! Umetumia muda na nguvu kiasi gani kutazama ndani. Kuangalia ukuta na paa la hema.

 

Kuangalia nje ndiko kulikomfanya Musa aache kutembea na wanadamu , aliacha kutembea mbele ya watu; akaishia kutembea juu ya watu. Alipopanda juu yam lima aligundua kwamba ukiwa kiongozi unakuwa kiongozi unapoona ng’ambo kuliko kuangaliana na watu.

Angalia nje ya ulipo.

Tumeshaona ALIKOTOKA-Kwamba alitoka Uru kisha Misri. Akiwa Misri nusura apoteze mke. ALIPOKUWEPO ni Bethel lakini yuko na Lutu

 

Sasa Mungu tizama nje kutokea ULIPO. Sehemu zako tatu zimejifia ndani yako unapoinua macho kutazama

 

Kutazama nje ya ulipo inahusisha maono ya huduma kiulimwengu, lakini lazima ufahamu haya kuhusu maono;

* Huwezi kuona umbali usioweza kuugharamia il kufikia

* Huwezi kuona umbali unaozidi rasilimali ulizo nazo

* Umbali unaoona una uhusiano na chakula unachokula au kulishwa

* Huwezi kuona umbali ambao macho yako hayafiki

Haya yote yako ndani yako.

 

Nataka uwe na maono ambayo watakaokuona waseme “asingekuwa Bwana…”

 

Kila kitu unachoogopa kina uhusiano na ulipo. Mungu hahangaiki na ulipo bali anahangaika na kule unakoenda.

 

Mungu hakuja maishani mwako ili ukae kwenye gari uliloegeshwa ili umwambie hali ya hewa ya mahali ulipo

 

Sababu ya Mungu kutojibu maombi yanayohusiana na ulipo ni kwa vile anataka kukuonyesha unakoenda.

 

INUA MACHO YAKO UANGALIE KUTOKEA ULIPO

 

Kuona ambako hujafika

Maono hukufanya kuandaa kikosi cha kutekeleza maono. Yote uliyofanya peke yako ni mema sana, lakini kwa ajili yale ambayo Mungu anatarajia kukufanyia utahitaji watu wa kufanya nao huduma. Watu waliojitoa ili kuleta matunda, wanaoweza kufanya kwa niaba yako pia.

 

Unahitaji watu wenye uwezo maeneo ambayo wewe huna uwezo.

 

Muulize Mungu niangalie upande gani?

 

Unataka niende wapi? Nyamaza kimya!

 

Unakumbuka alimwambia Ibrahimu?

 

Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi

 

Sio njia moja tu, bali Kaskazini, kusini, Mashariki, Magharibi x4

 

Watu wanaweza kukufungia uende upande mmoja au ukae kwenye hema lakini Mungu anakuoneysha wapi?

 

Mungu anakupa wapi?

 

Mungu anakutuma wapi?

 

Kanisa hili nataka liende kila mahali, Huduma yako iende kila mahali. Huduma yako isiishie Kanisani tu

 

Walio na afya hawahitaji tabibu

 

Huduma yako inahitaji kwenda magerezani, Inahitaji kwenda kwenda nyumba za kulelea watoto, Inahitaji kwenda kwa yatima, wajane na wazee. Iende ulimwenguni mwote.

 

Kanisa linatakiwa kuwa la ulimwengu, linatakiwa kuwa kwa ajili ya ulimwengu

 

Kanisa lisikike radioni, liwepo kwenye television, liwepo kwenye hospitali, kilimo, Elimu, kwenye biashara na uongozi

 

Unahitaji kuwepo serikalini, uwepo kila mahali-Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi. Unapaswa kwenda ulimwenguni mwote.

 

Kanisa lina nafasi gani kwenye jamii? Kanisa linafanya nini kwa ajili ya jamii?

 

Yote haya yanawezekana kama unaweza kufanya huduma nje ya hema yako, nje ya kabila lako, nje ya kijiji.

 

 

KUKWAMA KUNATOKANA NA KUIMBA WIMBO TUNAOUFAHAMU

Yesu aliposema mmoja kati yenu ni Ibilisi. Wanafunzi wake hawakuanza kushangilia kwa sababu walichokisikia hawakukijua kabla. Leo Kanisa linashangilia linaposikia walichokijua kabla. Wakisikia kipya watanyamaza, hawatashangilia.

 

Kila mwanafunzi alianza kuuliza, Bwana, ni mimi? Nashauri kila aliyeketi hapa anajiuliza kama tuliyofundishana yanamhusu. Ukiona hujiulizi labda wewe ndiye.

 

Moja ya makosa makubwa kwa mfanyabiashara kufanya ni kuhisi wateja wote wanafanana na yeye. Ndipo unajumua bidhaa unazozipenda

 

Lazima ujifunze kwa nini Wakorea wanatenengeza nywele ambazo wanauza Africa. Hawavai mawigi lakini wanauza.

 

Mungu akikuweka kwenye mji lazima utafute kitu kinachogusa mahitaji ya mji. Lakini vizuizi na vikwazo vinalifanya Kanisa libakie lilivyo kwa kuimba na unashirikiana na wanaofanana na wewe na unapata kilekile. Unaangalia ulipo

 

Kuna watu kwenye mji ambao hawawezi kufaidika na viapawa alivyokupa Mungu. Kuna watu kwenye mji kama watasikia mafundisho unavyofundisha watapokea kuliko wale wanaofanana na wewe

 

Huwezi kujua hadi utupe mkate kwenye maji

 

Huwezi kujua kwa kuendelea kutunza mkate

 

Tupa mkate kwenye maji uone Mungu atakachofanya

 

Toka kwenye mazingira uliyozoea

Nenda ambako Wahubiri wenzio hawaendi. Hutubia wale ambao Kanisa lenu halijazoea kuwahutubia. Badala ya kuimba kwenye kuta za hema nyimbo zako tuzisikie kwenye mabasi, masokoni, na sehemu mbalimbali. Mahubiri yako yasikike radioni na kwenye magari

 

 

TAZAMA KUTOKEA HAPO ULIPO

Kisha akamwambia “inuka uende”

 

Hili ndilo somo la Kongamano letu

Uzuri wa Kongamano hili sio bajeti, sio kujaa watu, sio vigelegele na sio mtu anapochinjwa rohoni bali ni pale hutaondoka kama ulivyokuja. Utakapoanza kutembelea kule ulikokuona, Utakapoanza kutembea kwenye maono.

 

Yatembelee maono.

 

Ukiweza kuona utaweza kufanana na unachoona, nataka uanze kutembea kwenye maono.

Usingoje watu wakuite majina ya maono wakati huendi kutembelea.

 

Umekuwa ukingojea kibali kwenda kuhubiri gerezani, Mashuleni, n.k

 

 

Mungu anasema nyanyua mguu ukanyage unakoangalia, tembelea. Tembelea maono

Tembelea kesho ya huduma yako, Tembelea anakotaka kukupeleka Mungu.

 

Kama unataka kuhubir magerezani tembelea magereza

Kama unataka kuimba tembelea studio na radio na television

Kama unataka kuhubiri mikutano ya hadhara tembelea mikutano ya hadhara na viwanja, shika shika vipaza sauti

Kama unataka kuhubiri radioni,magazetini, tv tembelea

Kama unataka kuhubiri masokoni tembelea viongozi wa soko

 

Tembelea maono! Ukingoja utumwe na mtu utajikuta unatembelea maono yake. Tembelea maono yako, Onyesha kwamba maono yako yanazaa ndipo watu wengine watakuunga mkono na kukusaidia. Usiombe msaada wakati wewe mwenyewe hujatembelea maono yako

 

Nenda Mamre kwanza!

 

Tembelea Mamre aliyokwambia Mungu moyoni mwako. Anza kutembea. Wale uliwaacha kwenye kijiji wataanza kusema hujui unakokwenda, umesahau asili yako, umeacha misingi waliyokuwekea, utachukiwa, utazushiwa, utasalitiwa, utaachwa.

 

Kama huko tayari kubeba msalaba huu usiandike notisi.

 

Kama hujali watakachosema, watakachokufanyia, watakavyokuumiza basi baada ya kongamano hili nenda Mamre. Huko utamiliki Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi

 

Naona watu wawili wanaanza kutembelea Mamre baada ya kongamano. Mmoja namwona anatamani leo aende Mamre!

 

Inuka! Tembea sasa! Tembelea unachoamini, tembelea unachoonyeshwa na Mungu, Tembea katika kile alichokuitia Mungu ufanye. Tembelea isiyoonekana. Tembea ndani yake

 

Unaona nini?

 

Unaona jingo kubwa la Kanisa, tembelea jingo hilo!

 

Halionekani!

 

Imani ni kuwa na hakika………

 

Ukienda atakupa, usienda hakupi.

 

Watasikiaje pasipo muhubiri……

 

Ukiingia mwezi mpya Mungu amekupa ili uingie Mamre. Uhubiri na kumiliki kimwili na kiroho kaskazinin, Kusini, Mashariki, Magharibi

 

Sema…Kaskazini…

 

 

Tena………

 

Neno la Mung kwa Ibrahimu linasema……Mapana na marefu

 

Kwenye marefu kumejificha Kaskazini, Kusini,

Kwenye mapana kumejificha Mashariki, Magharibi

 

Kila mji unaoenda una marefu na mapana.

 

Neno la Mungu kwa ni kwenda au kukaa?

 

Kukaa nyumbani?

Kukaa kwenye banda la mazoea?

Kukaa kwenye viti vya kanisani?

 

Ninapomaliza nataka unisikilize vizuri, unielewe vizuri bila kuangalia picha za kwenye flash ya mwaka 2010

 

Neno la Mungu kwako ni kwenda ulimwenguni mwote

 

Kutoka nje ya hema ya mazoea

 

Neno la Mungu kwako ni huku sio kule. Huku hakujaboreshwa ila ni kupya!

 

Neno la Mungu kwako ni kwenda alikokuonyesha

 

Neno hili sio kwa ajili yako, bali neno la Mungu kwako

 

Kwenye hema watoto kama nyota hawawezi kutosha,

Kwenye hema watoto kama mchanga hawawezi kutosha

 

Kinachokufanya uendelee kukaa kwenye ni vile Lutu alikuwa hajondoka

Ni vile watoto kama mchanga bado hawajafika

Ni vile watoto kama nyota hawajafika

 

Hayo yanazuiliwa na mazoea mawili:

  1. Lutu
  2. Hema

Watoto wako wanategemea maamuzi yako leo ya kuachana lutu, maamuzi yako ya kutoka nje ya hema

Kuongezeka kunakungoja uamue leo

 

Baraka zinangoja maamuzi yako leo

 

Wakati Ibrahimu yuko ndani ya hema nchi yenye mapana haikuwa kwenye hema. Kwa kadri unavyoendelea kukaa kwenye hema lako mapana ya kumjua Mungu hayawezi kuingia kwenye hema

 

Ahadi ya kuzaliana hutaipata kwenye hema

 

Unatakiwa kuangalia nje ya hema ili wazao wako wasirithi hofu yako,

 

Wasirithi woga wako!

 

Ili wawe na upeo mkubwa kuliko upeo wako

 

Ili kuuhamisha uzao wa Ibrahimu Mungu alimhamisha Ibrahimu

 

Kwa hiyo neno la Mungu kwako ni kwa ajili ya wote wanaokusubiri nje ya hema

 

Ni kwa ajili ya wote wanaokubiri nje ya kijiji,

 

Wanaokusubiri nje ya mazoea, nje ya dhehebu (dhehebu ni kundi linaloamini biblia lakini lakini halifuati neno la Mungu, linafuata mazoea), Ni kundi lililojaa hila na vita,

 

Kuna watu wanakusubiri nje ya ushirikiano na umoja unaokuzunguka, nje ya kawaida yako,

 

Ulimwengu unakusubiri umwondoe Lutu

 

Kuna mahali Mungu ameandaa sio tu kwa ajili yako bali kwa ajili ya wanao.

 

Hii inaitwa Baraka za kizazi (generational blessings). Baraka kwa wazao wa kimwili na wa kiroho

 

Mungu anakemea akili nyembamba, akili inayofikiri ulipo.

 

Nyamazisha roho ya kushindwa

Kemea kwa sababu akina Ibrahimu wengi tuko hapa tumefungwa kwenye kuta za hema

 

Huu sio wakati wa kushindwa, huu ni wakati kutembea kwenye maono. Kongamano hili likiisha kila kitu chini yako kianze kutembea

 

Jiandae kwa mabadiliko, Jiandae kwa ajili ya kusonga mbele.

 

Simama, mshike mkono jirani yako!

Roho wa Mungu yuko hapa, Roho wa Mungu yuko mahali hapa

Unatakiwa kuanza kufikiri ulimwengu na sio hema

Ondoka kwenye fikra nyembamba

Mungu anataka kukupa mlango wa kimataifa, mlango wa kiulimwengu

Mlango mpana

 

Kaskazini, Kusini,, Mashariki, Magharibi utaenda

 

Jiandae kuhubiri sehemu ambazo hujawahi kwenda kuhubiri

 

Hujawahi kuitwa kufundisha,

 

Utaandika vitabu, utarekodi mahubiri

 

Nenda ulimwenguni, nenda makanisa

Yesu alienda kwenye masinagigi,

Paulo alienda kwenye masinagogi

 

Roho wa Mungu atupaye uzima atupe uzima wa macho

 

Kila utakalogusa, kila mahali miguu yako itakapokanyaga, kila unalokanyaga, Mungu amekupa

 

Watoto wako wa kimwili na kiroho wataishi kwenye nchi mpya kwa sababu yako

 

Panuka, nenda ulimwenguni, nenda ulimwenguni

 

Tuombe:

In series Mahubiri