All Sermons
Bible Passage Yakobo 5:16
This content is part of a series Mahubiri, in .

Moto wa Maombi

Date preached April 9, 2025

Utangulizi:

Maombi ni pumzi ya kiroho. Mtu asiyeomba anaishi maisha ya kiroho yaliyokufa. Biblia inatufundisha kuwa maombi ya mwenye haki yana nguvu ya ajabu. Tuna mifano mingi ya watu waliogeuza historia kwa maombi – Eliya aliomba mvua isinyeshe, na haikunyesha miaka mitatu!

Mafundisho:

  1. Maombi ni njia ya kuwasiliana na Mungu – Bila maombi hatuna mazungumzo na Baba.

  2. Maombi huleta mabadiliko – Yakobo 5:16b, “Maombi ya mwenye haki…”

  3. Maombi hujenga uhusiano wa karibu na Mungu

  4. Maombi huweka ulinzi wa kiroho – Yesu alisema “Ombeni ili msijaribiwe.”

Maombi:

“Ee Bwana, nirejeshee moto wa maombi. Niponye kwa uvivu wa kiroho. Nijaze kwa hamu ya kukaa mbele zako kila siku.”

Hitimisho:

Moto wa maombi hautakiwi kuzimika. Tambua kuwa ushindi wako unategemea madhabahu yako ya maombi. Anza leo – anza tena!

In series Mahubiri