Ni muhimu sana kufahamu somo hili linalohusiana na mkate na hema ya kukutania kwa sababu nafahamu kwamba ni vigumu kumfahamu Yesu na kulifahamu neno kama huelewi hema ya kukutania.
Wengi wanafahamu hadithi za Biblia lakini wakati fulani ni vigumu kujua zina maana gani
Wote tunajua Yesu alienda msalabani lakini unaweza usijue kwa undani kwamba damu yake ilikuwa ni muamala wa kukununua
1Wakor. 6:19
Kwa hiyo unajikuta unatumia maneno kama ukombozi, lakini hufikirii kwa undani maana yake
Ni hadi unapoenda kwenye hema ndipo utaona damu juu ya madhabahu
Ndipo unapotambua kwamba Yesu alipopaa ilikuwa muhimu apae kupita mawingu hadi Pa patakatifu pa PatakatifuI have done it
Hema ilijengwa jangwani mwaka mmoja baada ya pasaka. Mwaka mmoja tangu waisraeli watoke Misri
Mungu alimwambia Farao waachie watu wangu wakaniabudu. Ujenzi wa hema ulikuwa ndio mwanzo wa kusudi la Mung kuwatoa Misri
Ni lazima ufahamu kwamba kuanzia Mwanzo na kuendelea anachotaka Mungu ni kuwa na mwanadamu
Mika 6:8
Aliweka bustani ya Edeni ali awe na mahali pa kukutana na mwanadamu
Alituumba kwa mfano wake ili tuwe na ushirika naye sio dini
Watu wengi wana dini lakini hawana ushirika na Mungu. Mungu anataka tuwe na ushirika naye
Aliiumba dunia ili apate kukaa nasi kwa ushirika
Alipofika bustanini na akaona mwanadamu hayuko kwenye ushirika akasema Adamu uko wapi?
Katika somo hili tunaangalia Kutoka 25:8
Yohana 14:1
Waebrania 9
Kwa kuwa hamuwezi kupanda juu basi Mungu aliwambia wana wa Israeli kwamba yeye atashuka na kukaa kati yao
Aya nyingine ninayotaka tusome ni Zaburi 91:1,9
Somo hili litasaidia kukua kama Mtumishi na kuhani.
Tukiacha kwenda kanisani kama kikundi cha kufa na kizikana na tukaanza kuja kanisani kama mahali pa kujifunza Neno la Mungu tunajifunza kwa umakini
Zingatia tofauti tunazoziona katika aya hizi;
Kutoka 25:8 Nijengeeni hema nipate kukaa kati yenu
Zaburi 91:1 Mungu akikaa kwenye hema haina faida kama wewe hukai naye
Kuna mambo unayapata kwa kutembelea na kuna mambo makubwa unayapata ukikaa naye
Unatakiwa kumtembelea Mungu unapokuwa na shida kwa sababu faida halisi zinapatikana unakaa naye
Sasa tuone mstari wa 9
Hiyo sio ahadi kwa wanatembelea kanisa. Ni ahadi kwa wakaaji, walio imara.
Unaweza kumshangilia Mungu ukiwa unaumwa?
Ukiwa umefilisika?
Ukiwa kwenye mgogoro?
Kumbukumbu 29:29
Bwana huwapa siri wale wamchao
siri hizo hawezi kukupa hadi ukae naye
Nikiwa kwenye hali mbaya nikae, Nikipitia wakati mgumu nikae, Sitambelea Mungu ila nitakaa
Wana wa Israeli walijenga hema zao kwa kuizunguka hema ya kukutania ilikuwa katikati. Mungu alikaa katikati yao
Kabla ya kujenga hema walikuwa
wanakaa chini ya wingu na nguzo ya moto
alikaa kati yao hema ilipojengwa (anakaa karibu zaidi, sio winguni, bali aridhini)
Wakati watu wengine wako hemani, wanaume walikuwa wanaingia kwenye behewa ili wamkaribie Mungu
Kuna watu hapa wako kwenye behewa. ni sawa, usihofu maana hata somo letu sasa tuko kwenye behewa
Behewa. Ufunuo 11
Hapa ndip palikuwa na Madhabahu ya shaba na birika ya shaba (brazen altar)
Hapa ndipo dhambi zilikuwa zinashughulikiwa.
Kwa hiyo, tunaona Mungu yuko mbinguni anamtuma Musa
Jangwani Mungu anakuwa na katika wingu na nguzo
Hema inapojengwa Mungu anashuka ardhini na waisrael wanajenga hema zao kumzunguka
Miili ya Wakristo ni maskani iliyozunguka Mungu na Mungu amezunguka. Mungu ndani yako nao ndani ya Mungu
Kwenye behewa ndipo wanyama walipochinjwa, ni eneo lilijaa damu kwa sababu hapa wanadamu na wanyama waliingia katika behewa
Wanyama walilipa bili za dhambi za mwaka mzima za wanadamu, Madeni ya aibu
Malipo yalilipwa kwa kutumia wanyama wasio na dhambi
Wanyama walitolewa uhai wao badala ya mwenye dhambi kutolewa uhai wake kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti
Unaona?
Ukombozi siku zote ni tukio la mbadilishano
Mungu alimwambia Adamu siku utakayokula tunda hilo utakufa, Kwa hiyo Mungu anapokuja bustanini ilikuwa amuue Adam au atafute uhai mbadala
Utakuwa unasema Adamu hakutakiwa kuuawana Mungu kwa sababu alikuwa amekufa tayari, ndio
Lakini Dhambi ya Adamu ilikuwa na vifo vitatu
1. Kifo cha kiroho cha mtenda dhambi
2. Kifo cha kimwili cha Adamu
3. Kifo cha fidia (sasa nazungumzia fidia)
Mungu alitafuta mnyama ili afe badala ya Adamu
Ili Adamu awe hai ilibidi mnyama afe, Hii ni picha ya Golgotha
Katika Mwanzo kabla ya sheria ya Musa makuhani walikuwa mababa na kazi yao ilikuwa ni kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi za familia zao
Kwa hiyo kama sio baba huwezi kutoa sadaka
Kama sio kuhani huwezi kutoa sadaka
Hivyo, hapa Mungu anatoa sadaka ya kwa ajili ya dhambi kwa ajili ya adam
Hivyo kuhani wa kwanza ni Mungu
Mnyama ni picha ya Kristo kufa msalabani ili sisi tuioshi
Dhambi zangu ndizo zilizomuumiza msalabani. Hakufa msalabani kama Kristo bali kama……
Alikufa kama…..
Alikufa kwa niaba yangu ili niishi kwa niaba yake
Discuss: Wagalatia 2:20
Ndio maana Yesu alisema unapoomba “ombeni lolote kwa jina langu”
Unapoenda kwa Baba usitaje jina lako, usivae nguo zako hawezi kukuona wala kukusikia
Isaya 59:1-3
Kwa hiyo Mungu anapoangalia msalabani aliniona mimi na Yesu hakuwa msalabani ila mimi nili kuwa msalabani
Yesu=mimi
Mimi=Yesu
Kwa kuchubiliwa kwake mliponywa
Tukawa wazima sisi ni Yesu
Tulibadilishana. Tumebadilishana
Kinaleta wokovu muamala unafanyika madhabahuni
Unatupa dhambi zako madhabahuni
Tulimtupia dhambi zetu naye alitutupia haki
Nifuatilie vizuri utajua mengi
Hayo yote yanafanyika behewani sasa tuingie ndani, Patakatifu
Nataka uangale jambo muhimu kabla hajaenda mbali
1. Kadri unasogea kwa Mungu ndivyo kundi linapungua
2. Kila mtu aliweza kukusanyika nje lakini wachache waliweza kuingia behewani
3. Lakini ili uingie Patakatifu ulitakiwa kuwa kuhani
ìPitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani, ingieni katika nyua zake kwa sifa. Mshukuruni na kulisifu jina lakeî Zaburi 100:4
Kila mtu anaweza kusifu, Kila mtu anaweza kumshukuru Mungu
Si ndiyo?
Zaburi 150 YAHWEH
Lakini linapokuwa suala la kuabudu, Makuhani wanaweza kuabudu.
Unaweza ukawa mwimbaji ukaimba nyimbo nzuri lakini linapokuja suala la kupewa siri za Mungu ukawa giza
Mungu anaposema nasi tunamjua
Yohana 4:24
Biblia haisemi wasifuo halisi, waimbao halisi bali waabuduo halisi
Kuabudu ni zaidi ya Kusifu, ni zaidi ya kushukuru
Kadri unavyokaribia kwa Mungu kwa kuabudu ndivyo ukaribu wa kuongea naye unazidi
Nyimbo: nyimbo za sifa zinakuweka karibu na watu
Nyimbo za kuabudu zinakuweka karibu na Mungu
Unaimba wimbo wa kuabudi unapoingia patakatifu lakini unaimba wimbo wa sifa unapoenda kwenye behewa
Unaposhukuru: Asante Mungu kwa kunipa watoto
Kwa kunipa mke
Kwa kunipa pikipiki
Kwa kunipa nyumba
Unapoabudu unamrudishia Mungu heshima!
Kusifu ni juu ya matendo ya Mungu
Kuabudu ni juu ya Mungu alivyo
Mika 6
Sasa karibu Patakatifu, ndani ya hema kama wewe ni kuhani kweli.
Mwambie jirani yako tunaingia Patakatifu
Unatakiwa kuwa kuhani ili uingie Patakatifu
1Petro 2:9-11
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
Mwambie jirani yako tuingie
Unapoingia unaachana na nuru ya jua hicho ndio kitu cha kwanza
Unaingia kwenye nuru ya mafunuo, tumeacha mionzi ya jua sasa tunaingia ndani kwa sababu ukifunikwa unapewa mambo matatu
1. Nguvu
2. Ulinzi
3. Mahitaji
Makuhani lilikuwa ni kundi lililochaguliwa iliwaweze kuingia patakatifu kwa niaba ya watu. Hii ndio nguvu ya Mungu kwa wanadamu
Kuhani anapoingia ndani alikuwa anamwakilisha Mwanadamu na Kuhani alipotoka kuwaendea watu alikuwa anamwakilisha Mungu.
Ngoja nikwambie nguvu walizokuwa nazo makuhani
Kama Askari wa Rumi wangemsulubisha Yesu bila
1. Kayafa kuhani kukubaliana kifo cha Yesu ingekuwa ni Mateso, ingekuwa ni kusulibiwa asingekuwa dhabihu
2. Yesu kuwa kuhani ingekuwa ni mateso tu
Kama unateswa na kuhani mkuu hakubaliana mateso unayopata utakuwa unapata taabu tu
Kama unateswa na sio kuhani, unapata taabu tu
1Petro 4:14
Kayafa ndiye anaibadili kifo cha Yesu kuwa dhabihu. Kwa sababu kuhani mkuu ndiye aliyekuwa na uwezo kumfanya mnyama awe dhabihu
Yesu asingekuwa Dhabihu kama kuhani asingehusika. Hili ni jambo la kwanza
Pili, Yesu ni kuhani aisye wa ukoo wa Kayafa, hivyo maovu waliyokusudia yalikuwa mema kwetu
Kwa kutumia vigezo vya kidunia, tunamwona Kayafa kwenye kifo cha Yesu kuwa dhabihu
Kwenye vigezo vya kimbingu tunaona Yesu ni kuwa dhabihu
Ndiyo, ni mtoa sadaka na sadaka, ni mtoa dhabihu na ni dhabihu yenyewe
Hakuna achukuaye uhai wangu bali nautoa uhai wangu kisha nitautwaa
Kama hivyo kama kuhani vipi wewe?
Warumi 12
1Yohana 3:16
Tunapoingia ndani ya hema tunakutana na mahitaji yetu
Sala ya Bwana:
Hema ni mahali tunapopate mkate wetu, chakula chetu. Mkate haupatikani nje.
Ni mahal pa mkate. Mahitaji yetu ndio muhimu sana
Mahitaji ya wokovu wetu!
Meza ya mkate wa wonyesho huonyesha mambo mawili:
1. Mahitaji ya kiroho
Mungu ni Yehiva yire- Mbuzi wa kafara, Kondoo wa kuuawa
Mbadala wa dhambi zetu
Alilipa gharama ya dhambi ili tukae hapa tulipokaaa
Alilipa ili haki isituhukumu
Alinyangíanywa nguo ili tuvae nguo-Kondoo alichunwa ili Adamu avae ngozi
2. Mahitaji ya kimwil
2Wakor. 9:7-10
Mathayo 6:28-33
Tunapoingia kwenye hema tunaenda kwenye mkate, Mkate wa minguni
Damu tumenawa kwenye birika (labor), Nimezaliwa! Nimeoshwa hatia na aibu ya dhambi
Nimepita mahali pa mauaji, kila wakati wanyama walipoingina kwenye Ua wan je, walijua hawatarudi
Ua wan je ni mahali pa hukumu, mahali pa kuchinja.
Ni eneo la damu. Harufu ya damu kila mahali, ni mahali pa uzazi. Sasa tunatoka mahali hapo
Waebrania 6:1-3
Tatizo la kanisa, tatizo la watu wengi leo ni kukwamba kwenye ua. Wanakwamba wakiwa wanagombaniana mafundiso, wengine wamekwama kwenye ubatizo
Kubishania siku ya kuabudu, kubishania kama umeokoka ama la
Umeingia kwenye mkate au uko kwenye ua wa nje? Huko ndio kuna mafundisho ya mabatizo na na changizo, na mafungu ya kumi
Umefungwa kwenye ua wan je?
Huu ni wakati wa kuondoka kwenye hiyo hatua
Unahangaika na dhambi kwa sababu haijalipwa kisawasawa? Kama bado unazungumzia mambo ya Ubatizo, kutawadha bado uko kwenye behewa
Soma tena Ufunuo: 11
Waebrania 10:19
Bado una hofu na watu. Bado unaogo pa yaliyokupata kambini, Bado uko nje behewani
Ilitakiwa yawe yameishia kwenye madhabahu ya shaba, ilitakiwa uwe unaoshwa kwenye birika
Sababu inakufanya uwe hivyo ulivyo ni vile hujalipa vya kutosha, vile hujanawa kisawasawa
Tunahitaji kwenda kwenye ukamilifu
Soma tena Waebrania 6
1Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu; 2mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya milele.
Mwambilie jirani yako tuondoke, tuingie ndani.
Waebrania 6 inatuhimiza kuondoka na mkwamo wa mambo ya awali na kusonga mbele kwenye ukamilifu. Tusipofanya hivyo tunamsulubisha mwana Adamu mara ya pili na kumdhalilisha wazi wazi
Mwandishi anawaandikia Wayahudi walioanza kumwamini Yesu na kisha wakaanza kuona mashaka, wakaanza kuhitaji mafundisho ya awali
Ni muhimu ukaelewa hili, ni muhimu uijue Biblia yako
Tunatakiwa kuondoka kwenye Neema, twende kwenye utukufu, tunavuka viwango, tunaingina viwango vipya vya ukuaji
Kuna vitu vingi Patakatifu lakini naanza na meza ya mikate
Nataka nihakikishe unapata kila kitu
Madhabahu ya uani na birika vyote vilitengenezwa kwa shaba.
Tunapoingia ndani vitu vyote ni vya dhahabu
Weka akili kwamba tunatoka kwenye shaba tunaingia kwenye dhahabu
Tunatoka kuwa shaba tunaingia kuwa dhahabu
Dhahabu ni madinin yanayotunza hali yake hata ikiunguzwa. Thamani yake inazidi thamani ya shaba siku zote
Kama Waebrania isemavyo, tunapoingia ndani tunaend akwenye mambo bora. Unapozungumzia dhahabu, unazungumzia madini yaliyopita kwenye moto na kuwa mbele za Mungu
Kama ilikuwa dhahabu ilipoingia kwenye moto itakuwa dhahabu inapotoka kwenye moto
Kama ulikuwa umeokoka unapoingia kwenye majaribu utatoka ukiwa umeokoka unatoka kwenye jaribu
Kama ulikuwa Roho Mtakatifu unapoingia, utakuwa na Roho Mtakatfu unapotoka
Bwana anajua mapito yangu, Baada ya kunijaribu nitatoka!
Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu Ayubu 23:10
Nitatoka kama dhahabu. Jambo pekee utakalonifanyia ni kuunguza takataka na vumbi, huwezi kuunguza dhahabu
Hivyo ndivyo unavyotakiwa kusema unapokuwa unashambuliwa
Usipojua hali yako ulipoingina hutaijua hali yako unapotoka
MEZA YA MIKATE YA WONYESHO AU MEZA YA UKUMBUSHO
Kabla sijazungumzia mikate, Roho wa Mungu anaisukuma nizungumzie meza
Mikate lazima ikae mezani na Meza lazima iandaliwe
Unapokuwa na jaa kali na unafika nyumbani unakimblia mezani
Ndio maana watoto hawajui kwamba meza lazima iandaliwe
Meza ya mikate ya wonyesho ilitengenezwa kwa mbao za mshita
Kut. 25:23ìUtatengeneza meza ya mbao za mjohoro yenye urefu wa sentimita 88, upana sentimita 44 na kimo sentimita 66. 24Hiyo meza utaipaka dhahabu safi na kuizungushia utepe wa dhahabu.
Haikuwa meza kubwa kwasababu ilikuwa inabebwa wanahama
Mikate ilikuwa inatembea
Mti wa mshita unapatikana maeneo makame jangwani, ni imara.
Meza ilitengenezwa kwa mti unaopatikana jangwani na kupakwa dhahabu
Tunaanza kufika sehemu nzuri sasa
Niseme hili?
Mbao ya mshita-Waisraeli
Dhahabu-Mungu
Mbao ya Mshita ñWanadamu
Dhahabu-Mungu
Tunaingia kwenye agano lenyewe
Mungu anafanya uhusiano kati mti wa mshita na dhahabu. Kama ubao ungeungua ungeisha
Ubao ukiwa umepakwa dhahabu ukiuunguza hautaungua kwa sababu dhahabu imefunika
Iharibikayo inaoanishwa na isiyoharibika
Dhahabu inawakilisha Mungu na mbao inawakilisha mwanadamu
Kwa hiyo meza ilitokana na Mungu na wanadamu na ilikuwa inahama na watu
Meza ile ni mwili wa Yesu
Yohana 1:14
14Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli.
Yesu alichukua mwili (mbao) wakati yeye ni Mungu (dhahabu)
Wafil. 2:6
Oh, Mungu wangu, kumbe na msalaba ulikuwa ni mti uliobeba mti. Msalaba ni ubao uliobeba ubao
Kumbe msalaba anaosema Yesu niubebe inawezekana ni tofauti na ninavyofahamu
Mkate ulikuwa unahama jangwani
Makuhani walikuwa wanabeba meza ya mikate ya wonyesho
Ilikuwa ni lazima Yesu awe ubao. Yeye kuwa mbao ndiko kulikomfanya awe ndugu yangu. Ndiko kulikomfanya awe mwana Adamu
Ilikuwa ni lazima avae mwili wa kuahribika ili aguswe na hisia za madhaifu yangu
Kama meza ingetengenezwa kwa dhahabu tupu asingeweza kunisaidia katika kuomba kwangu
Warumi 8:26
Ali awe mwokozi wa ndugu zake aliutwa hali ya utumwa na Mungu alitengeneza meza kwa kutumia mti ili atuokoe kwa kutumia mti.
Kwa hiyo, Mwanadamu amewakilishwa na mti wa mshita, na Mungu amewakilishwa na dhahabu
Katika mtazamo wa agano jipya
Kwenye meza ile unamwona Yesu akiwa mti wa mshita na anakuwa dhahabu ili awe Imanueli Mathayo 1:21
Hiyo ni meza ya mikate ya wonyesho!
Oh Mungu wangu nihurumieÖ jambo hili ni zito!
Yesu anapozaliwa alizaliwa Behlehemu
ìnyumba ya mikateî
Mikate haikutakiwa kutolewa mezanix3
Mikate 12 (3×4)
Kuna kitu kipya nimepata, nje Waisraeli wameizunguka hema kambi 12 ndani ya hema kuna mikate 12 mezani nayo ilikuwa mzunguko
Wakati wa chakula cha mwisho kabla hajateswa aliketi chakulani yeye na mitume 12
Yesu ndiye mkate (chakula) wa kweli
Yohana 6:48
Waisrael walitembea jangwani na huku makuhani wanabeba vifaa vya hema
Miaka 40 nguo hazikuchakaa wala viatu havikuwaishia
Najiuliza pea za viatu ulizo nazo nyumbani
Idadi ya pea si muhimu, muhimu ni je safari inaendelea?
Tangu uzaliwe umevaa pea ngapi?
Inawezekana unaonekana husongi mbele lakini cha muhimu hurudi nyuma
Inawezekana inaoneka hujatoka lakini najua hujazama
Mungu hatakuacha jangwani, ataweka mlango wa kutokea
Huyo ndiye Mungu!
Alikuokoa ajali ilipotaka kkutoa uhai
Ajali zingine zinategenezwa na mapepo, kumbuka mawimbi ya baharini
Mawimbi hayataki uvuke lakini Mungu ameweka mlango wa kutokea
Sifanani na kule nilikotoka, ningekuonyesha nilokotoka wengine wangezimia
Ungeona kuzimu nilikoibuka ungenihurumia
Mwambie rafiki yako, bado nipo.
Kansa haijaniua
Njaa haijaniua
Lukemia haijaniua
Kisukari cha mapepo hakijaniua
Wachawi hawajaniua, bado nipo!
Una watu waliokuacha? Ambao walidhani bila wao utakwama?
Wapigie leo wambie bado nipo
Jipige picha watumie waambie bado nipo
Inawezekana uko jangwani lakini Mungu amekupa uziia japo uko jangwani
Kila ni k ifikiria wema wa Yesu na maumivu aliyopata, Napata nguvu ya kumaliza jangwa langu
Hata kama unapita katika jangwa gumu kiasi gani leo kuna mkate waliokula Waisraeli
MAANDALIZI YA MKATE
Mikate ya wonyesho haikuandaliwa na Mungu lakini ilitegenezwa kuwa kufuaata maelekezo ya Mungu
Meza ya Bwana inaandaliwa na wanadamu lakini kwa kufuata maelekezo ya Mungu
Kwa hiyo utengenezwaji wa mkate ni matokeo ya jitihada ya pamoja kati ya Mungu na mwanadamu
Mungu alitoa viungo, mwanadamu alitengeneza mkate
Lazima ujue kwamba unga wa mkate haukununuliwa tu dukani
Mkate ulitengenezwa kwa ngano iliyosagwa kwa mawe yaani ngano ambayo haijakobolewa
Unga wa dona ya ngano. Haukutakiwa kuwa unga wa keki ambao ni laini. Unga huu Mungu anauita unga safi
Mikate ilikuwa 12.
Mhh,, mikate inawakilisha watu
Kwa hiyo watu ni mkate na Yesu ni mkate
Unataka cheo wakati hutaki kuwa mkate. Mkate uliotokana na unga ulioburuzwa na mawe
Hujawahi kuwa mkate kwa sababu unataka cheo
Hakuna taji bila mijeredi
Unakuwa mkate baada kuburuzwa na mawe
Mathayo 26:26
Mungu anataka kukufanya mkate anakumega, anakuvunja kiburi, anavunja ubishi na ukaidi
Anakubadili kuwa majivu
Ndio, anakunyenyekeza
Kukufanya useme Amen kwa ajili ya mapenzi yake
Kuna wengine wanapitia magumu maishani kuliko unayofikiria, huo ndio wakati Mungu anakusaga uwe unga wa mkate
Unapitia magumu hadi unga wako una chumvi kwa machozi uliyotoa, mkate wakati mwingine unahitaji chumvi ili usioze
Umepitia upweke, na ukiwa na maumivu. Bwana amekuleta hapa leo
Ili ujue mkate
Kwa hiyo, mikate 12 ilipokuwa juu ya meza ilikuwa ni watu wa Israeli wakiwa mbele za Bwana usiku na mchana .
Kinachonipa furaha ni kwamba sio tu Mungu alijiweka kama mkate bali pia wana waisrael walikuwa mbele za Mungu kama mkate na wote walikuwa mezani
Warumi 12:1
Jambo la kwanza ninalotaka ujue ni kwamba:
1. Uko mezani pa Bwana
Majaribu, na taabu zote ulizopata zimekuwezesha kuwa chakula cha Bwana
Haijalishi unaomba kiasi gani maombi hayabadilishi mchakato wa Mungu juu yako.
Hakuna wakati meza ilibaki bila mikate
Mkate ulikaa wiki nzima na kubadilishwa siku ya sabato wakati wa kufukiza uvumba
Kumbuka uvumba ni maombi ni sala za watakatifu
Na makuhani walikula ile mikate wakati inabadilishwa. Hata wakati hema haitembei mikate ilikuwa mezani
Namwomba Mungu siku zote meza yangu isiishiwe mkate
Watu wasije kanisani na kukosa mkate
Nyumbani mwa Bwana kuwe na mkate kila siku mezani pake
Mezani kwangu kusikosekane mkate
Ukiwa kanisani ujue kutofautisha mchuzi na chakula, makelele na chakula cha Bwana
Kanisa limepoteza utambuzi, chakula kinatupwa wanakula mchuzi
Chakula halisi hukutia nguvu
Badala ya kuwa na uchungu, kisirani, na maumivu, Mungu amekuleta ili uutoe uhai wako mezani pake kama naye alivyoutoa uhai wake mezani ili uelewe kwamba michubuko inakupa Baraka
Yohana 3:16
1Yohana 3:16
Michubuko inakuimarisha
Michubuko inamfanya msichana kuwa mwanamke, Michubuko inamfanya mvulana kuwa mwanamume
Huwi mwanamume kwa sababu umesherehea birthday nyingi
Unakuwa mwanamume kwa sababu umeenda kuzimu na kusimama dhidi yake
Wewe ni mkate wa Mungu kama dhabihu iliyo hai
Ee Mungu nisaidie nitoke hapa,
Upande mmoja una mkate umetolewa kwa Mungu na upande wa pili ni Mungu anatupa mkate
Kwa sababu anasema hataiacha meza yangu bila chakula
Yesu ndiye Emmanuel, Atakuwa nawe Wakati wengine wameondoka
Atakuonyesha njia
Atakuwa nawe kwenye mawimbi
Atakuwa nawe jangwani
Atakuwa nawe watoto wako wakiondoka
Atakuwa nawe marafiki wakiondoka
Mana inashuka kutoka mbinguni, Mungu anawalisha watu wake
Mkate wa mbinguni
Mungu hukaa kati yetu nay eye ndiye maskani yetu, na sisi ni masikani yake
Ni mkate wa uzima
Kwa nini bado unataka vitunguu vya Misri? Yeye ndiye chakula cha mbinguni
Si unaona ulivyoshiba?
Neno halisi la Mungu ni chakula.
Neno halisi litavunja pingu
Shetani ni mjinga
Anamwambia Yesu ìgeuza mawe ya mkateî
Yesu anageuzaje mawe kuwa mkate wakati yeye ni mkate?
Usipojitambua utachanganya mkate na jiwe
Sifa na utukufu kwa Bwana!
Weka mkate mezani pa Bwana.
Weka mkate