Kuhusu sisi

Falsafa ya masomo –Hii ni shule iliyoundwa ili kumpatia  mwanafunzi wa Neno la Mungu elimu ya Biblia kwa kina na mapana. Masomo yaliyopo ni yale yatekwayo kama maji kutoka kwenye Biblia. Masomo haya ni kwa ajili ya yeyote anayependa Neno la Mungu.

Walimu:

Walimu wote wanaofundisha na kuweka masomo hapa ni walimu wabobezi waliojifunza Neno la Mungu kwa miaka mingi na wamejiandaa vilivyo ili kukusaidia katika safari hii ya kujifunza na kusoma ramani ya moyo wa Mungu-Biblia. Ni miongoni mwa walimu mahiri kabisa ambao Kanisa limebahatika kuwa nao kwa siku hizi. Kiwango cha elimu inayotolewa hapa ni sawa au zaidi ya elimu itolewayo katika vyuo vya Biblia au seminari. Kila mhitimu ataweza kuwafundisha wengine kabisa.

Mkurugenzi wa Shule:

Mkurugenzi wa shule hii ni Mwalimu na Mwinjilisti Willy Emmanuel. Amekuwa mwinjilisti na muhubiri wa Injili kwa zaidi ya miaka 30. Amehutubia na kufundisha katika makongamano kadhaa wa kadhaa na Mikutano ya hadhara. Pia ameandika vitabu na majarida mbalimbali pamoja na video za mafundisho.