GLOBAL CHURCH OF CHRIST JESUS TANZANIA
IDARA YA UMISHENI NA ELIMU
Limeandaliwa na Willy Emmanuel
KAZI ZA KUHANI
1 Petro 2:10-12
4Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa. 5Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea tambiko za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.
9Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu. 10Wakati mmoja nyinyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa nyinyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa mmepokea huruma.
Asante fundi aliyenikataa! Asante kwa kazi ambayo sikufanikiwa kuipata
Asante kwa wote walionifukuza!
Ukimwamini Mungu hutatahayarika
Rudi soma mstari wa 8,9
Somo letu ni Majukumu ya Makuhani, Mungu anataka ujue kwamba wewe ni kuhani
Hii haikufanya kuwana dharau kwa wahubiri, wazee wa kanisa kwa kujiona sawa na wao
Waebrania 13:7,17
Neno kuhani leo linapotumika wengi wanalitumia kumaanisha wahubiri
Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
17Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.
Aya yetu inasema ìukuhani wa kifalmeî na Ukuhani mtakatifu
Wewe sio kuhani bali wewe ni ukuhani. Ni ofisi, wewe ni kazi yenyewe.
Tatizo ni pale tunaposhindwa kuuheshimu ukuhani.
Nirahisi kumsema kuhani mwenzio bila kujua unajisema na unaisema ofisi nzima
Unamvua nguo mwanaume mwenzio unajivua hata wewe
Kuhani kazi yake ni kumwakilisha Mungu anapokuwa na watu na kuwakilisha watu anapokuwa mbele za Mungu
Unamwakilisha nani unapokuwa mbele za Mungu?
Watoto wetu siku hizi wanaacha kanisa kwa sababu hawajafundishwa kutumika
Wamefundishwa maslahi u
Wamefundishwa kupokea, mara cha kupokea kinapoisha wanaondoka hata kama unawaona
Watoto siku hizi hawaoshi vyombo na unashangaa kwa nini mke wako anachoka
Huwafundishi
Lakini Biblia inasema sisi ni ìukuhani mtakatifuî. Sio kundi la waumini, sio tu kanisa, sio tu makuhani lakini ukuhani wa kifalme, Ukuhani mtakatifu
Tuna kazi tuliyoitiwa ambayo ni kutumika kama walivyotumika makuhani
Ukichunguza hema na hekalu, hakukuwa na kiti kwa ajili ya makuhani
Hakukuwa na pa kukalia
Hii kawaida ya kutokaa ni picha ya Mung mwenyewe. Sifa zilitakiwa kukwea mbele za Mungu daima,
Moshi wa sadaka ulitakiwa kufuka muda wote
Na bado tunaishi katika zama ambazo kazi tunayofanya ni kukaa
Na sababu huwezi kutumika ukiwa umekaa
MUNGU KUHANI WA KWANZA
Mwanzo 3:15
Biblia inasema Adam na Eva walisikia sauti ya Mungu bustanini
Sauti ya Mungu ndio neno la Mungu
Neno la Mungu ni Yesu
Ni lazima uelewe kwamba Mungu aliacha kupumzika na kuinuka ili amtumikie mwanadamu aliyeshindwa kumstumikia
Alishuka ili amtumikie mtumishi wake
Na anaposhuka alishuka kama kuhani
Alimjia Adamu kwa sababu alishindwa kwenda kwake
Tuna Mungu anakuja kwako unaposhindwa kwenda kwake
Si Adamu aliyemtafuta Mungu bali Mungu alimtafuta Adam
Hapa tunaona ukuhani mtakatifu kwa mara ya kwanza
Mungu akafanya ngozi ya mnyama na kumfunika mwanadamu
Damu inamwagika na mnyama anakufa
Muda wote Mungu anapomchinja mnyama, anachuna ngozi Adamu alisimama tu kwenye dhambi
Kwa sababu hawezi kumsaidia Mungu kumwokoa
Mungu ni kuahani wa kwanza tunayemwona katika Mwanzo na ni kuhani wa mwisho milele na milele
Unajiuliza kwa namna gani?
Yohana 3:16 Mungu alimtoa mwanawe wa pekee
Yohana 1:39 Yesu ni mwanakondoo wa Mungu
Hivyo Mungu ni kuhani alimtoa mwanakondoo kuwa dhabihu
Katika Agano la kale wanyama waliokuwa wanachinjwa walikuwa nembo ya Yesu na hivyo Yesu alichinjwa katika agano la kale na kwa hakika alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu
Mungu ndiye mwanzo na mwisho
Yesu ni kuhani pia kwa sababu ni mwana wa Mungu aliye kuhani. Kwa jinsi ya dunia
Mungu hajakuokoa kwa sababu una degree,
Hajakuokoa kwa sababu ni mzuri
Sio kwa sababu unaimba
Sio kwa sababu unahubiri vizuri
Alikuokoa kwa sababu yeye ni mtakatifu
Amekufanya uwe mteule
Kuna watu ni wazuri, lakin alichagua wewe! Alikusitiri
Umefika leo sio kwa sababu huna dhambi, bali kwa sababu amekustiri
MABABA NI MAKUHANI WA PILI
Kutoka kwa Mungu ukuhani ukwaangukia wanadamu
Sura ya nne tunamwona Habili na Kaini wakitoa sadaka
Habili anauawa kwa sababu ya majukumu yake ya kikuhani
Mathayo 23:35Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kumwagwa damu ya Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka ile ya Zakaria, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
Sio tu Kaini alimuua Habili bali shetani alikuwa anajaribu kuua ukuhani
Kwa sababu ukuhani unawapatanisha wanadamu na Mungu
Alipomuua Habili damu iliendelea kulia
Alikufa lakini bado alikuwa ni kuhani. Moyo wake ualiacha kupumua lakini damu ilikuwa inaongea
Habili aliishi kama kuhani, alikufa akiwa kuhani Waebrania 12:24; 11:4.
Kwa nini Kaini alimuua Habili? Kwa sababu alikuwa kuhani, hakuiba, hakusema uongo, hakulewa bali sadaka zake zilipokelewa
Kwa nini Yesu aliuawa, alikuwa ni kuhani
Watu wanakuchukia kwa sababu unampenda Mungu,
Wanakuchukua kwa sababu unafuata ukweli wote
Mungu amekuokoa na wanakuchukia kwa sababu hujajiua
Waebrania 13:15
Sababu ya shetani kukuchukia hivi ni kwa sababu ameshindwa kukunyangíanya sifa mdomoni mwako. Yeye alikuwa malaika wa sifa, sauti yake ilikuwa nzuri
Hapendi uwe na sauti nzuri ya kumwimbia Mungu
Anataka uimbe kivivu
Alipoanguka, nafasi ilikuwa wazi, Mungu amekupa nafasi yake umwimbie sifa na huimbi?
ìNa tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, tunda la midomo yetuî
Sifa ni dhabihu
Miili yetu ni dhabihu
Yesu ni dhabihu
Kwanini usiwe kuhani?
Ni lazima uimbe hadi shetani akuchukie
Mdomoni mwako mnatoka maji ya uzima lakin kuna mauti.
Kinywani mwako kuna uzima kwa ajili ya watu wa Mungu lakini mauti kwa ajili ya mapepo na shetani
Unatoa sifa, unatoa dhabihu ya sifa unatoa mauti kwa shetani lakini unakuwa faraja, unakuwa maonyo, unakuwa nguvu kwa watu wa Mungu
Zaburi 66:1
1Enyi watu wote duniani mshangilieni Mungu!
2Imbeni juu ya utukufu wa jina lake,
mtoleeni sifa tukufu!
3Mwambieni Mungu: ìMatendo yako ni ya ajabu mno!
Nguvu zako ni kubwa mno hata maadui zako wanajikunyata kwa hofu.
4Dunia yote inakuabudu;
watu wote wanakuimbia sifa!î
Tunapoimba tunatoa sadaka
Tunapoimba tunaunguza dhabihu
Tupoimba tunatekeleza majukumu ya ukuhani
Malaki 2
8ìBali nyinyi makuhani mmegeuka mkaiacha njia ya haki. Mafundisho yenu yamewaongoza watu wengi katika kutenda mabaya. Mmelivunja agano nililofanya nanyi. 9Nami pia nitawafanya mdharauliwe na kupuuzwa na Waisraeli, kwa sababu hamkuzifuata njia zangu, na mnapowafundisha watu wangu mnapendelea baadhi yao.î
Soma na Malaki 1:13
Sema na mwenzio ìwewe ni kuhaniî Sadaka zako za sifa ni nzima?
Kama unahubiri unatoa sadaka kwa Mungu
Turudi kwenye eneo la somo letu
Ukuhani wa mababa
Mababa walikuwa makuhani
Nuhu alikuwa kuhani
Ile kuwa mtoto wa Nuhu au kuwa mke au mkwe wa Nuhu ilitosha kabisa kuwa salama
Umekuwa chini ya mbawa za kuhani
Hawakutakiwa kutoa chochote
Hawakutakiwa kubatizwa
Lakini kuwa familia ya Nuhu ilitosha kuwaokoa na gharika
Jiulize, unahusiana na nani? Uhusiano wako unaweza kukuokoa au kukupoteza
Unaendaga Kanisani jumapili tu?
Sio tu Nuhu alijenga safina kwa ajili ya familia yake lakini pia alijenga madhabahu kwa ajili ya shukrani
Unajua kwa nini baadhi ya watu ni vigumu kwao kujenga Kanisa? Unajua kwanini ni vigumu kujenga madhabahu?
Kwa sababu hawajui kama ni makuhani hata kama wana hela
Ukiwa kuhani utagharamia lakini pia haitakuwa vigumu kumwambia Mungu akubariki
Unashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya ujuaji wako
Unasema sio lazima, ni hiari, kwa kadri ya kufanikiwa
Kwa kadri unavyoendelea kuwa mjuaji ndivyo kiburi kinavyotafuna Baraka zako na suala la kutoa linaenda mbali
Ndio maana mambo mengi yamekwama, umekuwa mpokeaji tu.
Unavunja sheria ya mbegu na mavuno. Kupanda na kuvuna
Hata kama huiamini biblia yako basi liamini neno la Mungu
Amini sheria asili ya mbegu
Kama kila siku unapokea na hujui kutoa, jifunze kwenye kupumua unakuwa hai kama unatoa pumuzi na hutoi utaugua, utakufa
Ulemavu wa kitabia
Ibrahimu alikuwa Kuhani
MWanzo 22
ìkule kuabuduî
Kwetu sisi ukisema naenda kuabudu tunarajia kukuona ukiwa umebeba Biblia ambayo huiamini
Umebeba tenzi ambayo huimbi
Sio lazima ubebe matoleo kama chenji za maandazi hazijabakia
Ukifika kanisani unasinzia- Kuhani anasinzia
Katika familia ya kuhani wakisema tunaenda kuabudu kitu cha kwanza kuja akili ilikuwa ni matoleo
Ni sadaka
Kabla hawafika mahali pa Ibada Isaka alimuuliza baba yake
Kuni zipo, kisu kipo lakini Sadaka siioni
Hii inaonyesha kwamba haikuwa mara ya kwanza
Hii inaonyesha kwamba kwenye nyumba ya Ibrahimu kulikuwana kawaida ya ibada, Kiasi cha Isaka kujua kinachokosekana
Watoto wengi hawaoni kinachokosekana
Hawakuoni unapoomba sebuleni, hawakuoni unasoma Neno la Mungu
Mara nyingi wanakuona unasoma Biblia
Ibrahimu alimchinja mnyama akaita ibada
Kama haombi mtoto ataombaje?
Haya yaliwezekana kwa sababu Ibrahimu alikuwa kuhani
Namna pekee ya kumfundisha mwanao kutoa ni wewe kujitoa kwa Mungu
Hiyo ndio nguvu ya baba aliye kuhani
Ibrahimu alitoa sadaka mbele ya Isaka na Isaka aliona
Ukuhani wa Ibrahimu uliwezesha Isaka kujua kinachokosekana
Anayefuata ni Melkisedeki:
Mwanzo 14:18Naye Melkisedeki, mfalme wa mji wa Salemu, ambaye alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, akaleta mkate na divai, 19akambariki Abramu akisema,
ìAbramu na abarikiwe na Mungu Mkuu,
Muumba mbingu na dunia!
20Na atukuzwe Mungu Mkuu,
aliyewatia adui zako mikononi mwako!î
Naye Abramu akampa Melkisedeki mchango wake sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo.
Zaburi 110:4 Mwenyezi-Mungu amekuapia wala hatabadili nia yake:
ìWewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.î
Waebrania 5:6-11; 6:6- 7;
1Huyo Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu, na kuhani wa Mungu Mkuu. Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka vitani ambako aliwaua wafalme, Melkisedeki alikutana naye, akambariki, 2naye Abrahamu akampa sehemu moja ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jina Melkisedeki ni ìMfalme wa Uadilifu;î na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia lina maana ya ìMfalme wa Amani.î
Kwa mara ya kwanza tunamsoma akiwa mfalme wa Salem na kuhani wa Salemu
Sasa tazama Kuhani Ibrahimu anakutana na kuhani Melkisedeki
Kwa nini Ibrahimu alitoa fungu la kumi kwa Melkisedeki wakati naye ni kuhani?
Ni swali ambao wajuzi wa Biblia wamejaribu kujibu bila mafanikio
Leo nataka ujue Neno la Mungu kwa ajili ya swali hili.
Ibrahimu alikuwa ni kuhani lakini hakuwa mfalme
Kwa hiyo alikuwa anatoa huduma za ukuhani wakati Melkisedeki alikuwa anafanya ukuhani wa ukuhani
Ukuhani na ufalme unapokutana ndipo ukuhani wa kifalme unatokea
Biblia inasema Yesu ni mfalme mfano wa Melkisedeki, ni kuhani kama melikisedeki
Biblia inasema sisi ni makuhani wa kifalme.
Kuhani wa kifalme anayefanana na Yesu ambaye anafananishwa na Wakristo ni Melkisedeki
Alitoa Mkate na Divai
Yesu usiku aliotolewa alitoa Mkate na Divai kwa sababu alikuwa anauanzisha ukuhani wa kifalme
Ndio maana tunashiriki meza ya Bwana. Kukuhani wa kifalme hutoa divai na makate
Alichokifanya Melkisedeki katika Mwanzo wa Agano la kale, Yesu alifanya mwanzo wa Agano jipya akiwa Yerusalemu usiku aliosalitiwa
Mungu anataka ufahamu kwamba wewe ni kuhani na ni mfalme
Hivyo tembea kama mfalme-mtawala Mwanzo 1:27-28
Tembea kama kuhani-Mtumishi wa Mungu na watu
Ukuhani wa kifalme
Unaitwa Melkisedeki
Mtu mwema anajua jinsi ya mfalme na jinsi ya kuwa kuhani
Tatizo tulilo nalo leo ni kwamba tunaona kama tunatakiwa kuchagua
Katika Kutoka 3:1; 18:5,12
YETHRO
Hapo Yethro, baba mkwe wa Mose, akamtolea Mungu sadaka za kuteketezwa na tambiko. Naye Aroni akaja pamoja na wazee wa Israeli ili kula chakula pamoja na Yethro, mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Musa alijifunza kuwa mfalme akiwa Misri lakin ili kuwa kuhani alijifunza kwa Yethro
Kuna mambo utajifunza kwa farao na mengine utajifunza kwa Yethro
Inachukuwa watu kumwandaa kuhani ambaye ni mfalme
Musa hakuogopa kwenda ikilu kumwambia Farao Mungu anataka uwaachie watu wake kwa sababu anajua ikulu ilivyo
Musa alijua kwenda kwa farao kwa sababu alifundishwa na Farao na alijua kuwaokoa watu kwa sabau amefundishwa na Yethro
Mungu anapokuita kutumika kama kuhani atakutuma kwa Yethro.
Unamjua Yethro?
Wengi wetu tumefundishwa na Farao lakini hatukubahatika kufundishwa na Yethro ndio maana hatuna unyenyekevu, hatuna kushuka, hatujui kuwa mtumishi ni kuwa mdogo
Alichokufundisha Farao kitakufanya ujue kutawala na sio kutumikia
Jihadhari na watu waliosoma kwa Farao
Ukuhani wa kifalme: Mungu anasema Wakristo ni ukuhani wa kifalme na sio kuhani wa kifalme bali ukuhani wa kifalme
Nakuhitaji uwe imara kama mfalme lakini nakuhitaji uwe mnyenyekevu ili unisaidie kutumika unapotakiwa kutumika
Nakuhitaji uwe kiongozi na mtumishi
UKUHANI WA WALAWI
Kuna tofauti ndogo kati ya kuitwa kwa haruni na kuitwa watoto wake
Hata kama alikuwa na watoto 4 lakini alipata upaka upako moja
Harufu ya watoto inafanana ya baba
Anachosema baba kinabaki na wewe
Mwanzo 49
Wakati waisraeli wako Sinai Lawi alikuwa ameshakufa
Simioni na lawi walilaaniwa
Musa alipokuwa mlimani, Haruni alitengeneza sanamu na watu wakaabudu wakiwa uchi.
Mungu akawaua wote ambao waliabudu isipokuwa waliochagua upande wa Mungu
Nataka uone kwa nini Mungu aliwaua
Walitengeneza sanamu iliyofanana na miungu ya Misri
Mungu aliwatoa Misri lakini Misri haikutoka ndani yao
Mungu hakushindwa kuwaingiza Kanaani bali wao walishindwa kuondoa mikate ya Misri ndani yao
Umeuacha ulimwengu lakini ulimwengu haujakuacha
Misri imetoka ndani yako?
Naweza kujua kwa jinsi unavyowatendea wengine
Naweza kujua kwa namna unavyovaa
Naweza kujua kwa jinsi unavyoongea
Kwa jinsi unavyotukana wengine
Na ugomvi ulionao
Unaweza kuwa shemansi na bado ukawa unagombania mipaka ya mashamba
Kama unataka kuondoka Misri acha kuabudu sanamu za Misri
Walawi walisema sisi tutakuwa upande wa Bwana, tamko hilo lilimfanya awape urithi kwenye nyumba ya Mungu
Walawi walichukua msimamo wakati wengine wanasitasita
Nataka nikuulize leo
Uko upande gani?
Uko upande gani?
Ili Mungu akufanye kuwa kuhani lazima ujibu swali hili leo
Kazi imebaki kwako
Leo jione umekutana na ukuhani
Leo jione umekutana na ufalme
Leo jione kuwa taifa la Mungu
Kabla hujasema lolote, kabla hujafunua kinywa chako
Tambua uwezo wa uzima na mauti uko kwenye ulimi wako
Kuna nguvu kubwa kwenye ulimi wako kiasi cha kuua huduma ya mwingine
Kwa sababu umekuwa kuhani, kwa sababu umewekwa wakfu
Anasema
Basi, acheni uovu wote;
Huruhusiwi kuishi na visirani, chuki
uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena
ìya kila namnaî
Huwezi kuona Uovu wote,
Huwezi kuona hula, Huwezi kuuona unafiki, huwezi kuuona wivu na masingizio
Mambo haya yapo kanisani lakini kanisa linahubiri mambo yanyoonekana
Kama una dhambi isiyoonekana uko huru kumsema mwenye dhambi inayoonekana
Kwa hiyo unaweza kusingizia na hakuna atakayekemea
Unaweza kuanza majungu nab ado ukawa unanena kwa lugha
Unaweza kuwa na wivu, unaweza kuwa mnafiki na unaweza kuna hila
Kwa sababu unaruhusiwa na dhambi isiyoonekana
Unaweza ukawa na hila alimradi hatukuoni ukiwa unazini
Kwa kadri ambavyo hatuiioni dhambi endelea kuifanya
Lakini nataka ujue kwamba kama unataka kuwa kuhani, Ili kuingia patakatifu ni lazima unawe kwenye birika
Mwanakondoo alichinjwa mahali ambapo pana madhabahu na birika
Madhabahu uliunguza kabisa ile sadaka ya dhambi na makuhani hawakuruhusiwa kuingia Patakatifu bila kunawa
Kwenye madhabahu kuna matendo ya dhambi, kwenye birika tuna tabia ya dhambi
Ni kwenye birika ndipo kuhani alitakiwa kukubali kwamba mikono yake ni michafu
Ndicho alichomaanisha Pilato aliponawa mikono
Katika Ezekiel 33 Nisipokuonya damu yako itakuwa mikononi mwangu
Kwa hiyo makuhani ambao walikuwa watumishi wa Mungu walipaswa kunawa
Hakuna mwenye haki
Kwa sababu wewe ni kuhani Mungu anasema ameguswa na chuki uliyonayo
Ameguswa na kisirani chako
Ameguswa na hila yako
Ameguswa na uongo wako
Chukua matendo yako ukawnawe
Sio kwamba umesema uongo, bali kwa sababu umejiepusha kuwa mkweli
Kuna mtu anaumizwa lakini unaujua ukweli husemi
Hiyo ndio hila
Umeacha watu wanaamini uzushi kwa sababu ya hila yakok
UNAFIKI: Umekuwa ukiwasema watoto wa wengine mpaka lilipokukuta na watoto wako. Sasa unataka kanisa liombe kwa ajili ya watoto wako
Wivu: Hapo ndipo tunapokutana na wenye chuki, unawakosa watu walikokuzidi wala hutaki kuwapongeza
Hizi ni dhambi zisizoonekana
Dhambi hizi zinaweza kuishi na wewe bila kutoka mdomoni
Ewe kuhani,
Mungu anasema wekeni mbali;
Kama kuna Baraka nitakayopata mwaka huu, natakiwa ninawe wmili na roho
2Wakor.7:1Basi, wapenzi wangu, tukiwa tumepewa ahadi hizi zote, na tujitakase na chochote kiwezacho kuchafua miili na roho zetu, tuwe watakatifu kabisa na kuishi kwa kumcha Mungu.
Kumbuka Waisrael walitangatanga jangwani mpaka wakafa kwa sababu ya mdomo
Walinungíunika na kulalamika kwamba heri wangefia Misri
Mungu akawapa mikate wakasema mana
Kila wakati Mungu anapotaka kukubariki anakutana na mdomo wako
Akimbariki mwingine unaanza mdomo
Unamsingizia, unamlaani, unamsengenya
Acha mdomo ubarikiwe
Sijui kama neno linakusaidia kama ulizoea kusaidiwa na Biblia?
MaandikoÖ
Wewe ni ukuhani wa kifalme!
Acha kuongea kihuni!
Umekuwa katika madhabahu ya shaba, Umempa Yesu maisha yako,
Amekusamehe kunyongwa kwako
Lakini mdomo wako uko kama Wamisri
Wakati mwingine sio mapepo yanazuia kubarikiwa bali na tabia zako ni kizuizi
Sio kwasababu hujaweka maisha yako kwenye madhabahu bali ni kwasababu hujasahau mabaya uliyotendewa na watu
Na unadhani kutosamehe kunamuumiza aliyekukosea lakini kutosamehe kunachelewesha Baraka zako
Mungu anavunjika moyo kila anapouona moyo wako
Leo ameniambia nikwambie
Yaache yote madhabahuni, piga hatua hadi kwenye birika ukanawe kisha ingia Patakatifu
Ameniambia nikwambie wewe ni ukuhani wa kifalme
Mungu anavunjika moyo anaoona hila
Anapoona hasira
Anapoona uongo
Kama kuna lolote ndani yako limekufanya uwe na uchungu hivi
Limekufanya usilale usiku
Linakufanya uwachukie watu Fulani
Linakufanya uumie kwa sababu wengine wamepewa cheo ambacho ulikitaka
Ni adui ameichachusha roho yako
Roho yako ina maambukizi
Mungu atakusafisha leo
Simama niombe na wewe
Mafuta ya Mungu yakufunike, yakutakase
Mafuta ya Mungu yakutie kimvuri
Mafuta ya Mungu yakuokoe
Wewe ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme