TWEKA KILINDINI
Luka 5:1-10
Mashua
Petro
nyavu
bahari/ziwa
samaki
Aya hii sio ngeni lakini kuna vitu ambavyo hujawahi kuviona kwenye aya hii hii Mungu ameniambia nikwambie
Yale ambayo Mungu anataka kufanya maishani mwako utahitaji usaidizi
Anataka kukupa kitu kikubwa kuzidi mashua yako
Waliokuja kumsaidia nao mashua zao zilianza kuzama
“Simoni Petro alipoona hivi alianguka akamsihi akisema ondoka kwangu maana mimi ni mwenye dhambi”
Somo letu ni “vunja vizuizi”
Kwa muda nilioishi nikihudumu katika Neno nimeshuhudia watu wengi wengi wakiamini na kubatizwa lakini wengi wao wanakosa maisha tele
Kuwahubiria na kuwabatiza sio mwisho wa kazi ya mwinjlisti kwa sababu kuwabatiza na kuwaacha wamekwama bila uelewa wa neno unakuwa hujawasaidia kuvuka vizuizi vinavyoweka ukomo wa maendeleo yao. Ni kama na wewe unasaidia wakwame
Wanapaswa kujua wao ni nani katika Bwana na jinsi ya kuzifurahia ahdi za Bwana
Nimegundua kwamba mara nyingi anachoamini mtu ni kipenyo kidogo cha jambo zima lakini kibaya zaidi anakuwa ameaminishwa kwamba hicho ndicho kitu kizima anachopaswa kujua na kuishi nacho
Ukweli kabisa ni kwamba mbali na baraka za rohoni pia kuna baraka za mwilini kwa watu wa Mungu na wengi wetu tunafanikiwa kupata za rohoni bila zile za mwilini
Ndani ya mtu kunakuwa na mifumo ya imani ambayo inaweza kukataa fursa ambazo Mungu ametupa
Biblia inasema Simoni alikuwa anaosha nyavu
Mifumo yake ya imani iliyojengwa juu ya mazoea na desturi ilikuwa imemwambia hakuna samaki
Mifumo hiyo hiyo ilimfundisha kwamba samaki wanapatikana usiku
Walikuwa wamefanya kazi usiku kucha bila kupata kitu
Mifumo ya imani ilimwacha akiwa amekikatia tamaa alichokihitaji
Kwamba usipopata usiku hupati kabisa
YESU ANAKUTANA NA WAVUVI WALIOKATA TAMAA
Yesu alipokutana na wavuvi waliochoka walikuwa wanaosha nyavu jambo ambalo ni uthibitisho wa kukata tamaa
Na leo anakutana na wewe unaosha nyavu umekata tamaa lakini pia umechoka
Nataka nikuonyeshe kwamba Yesu aliyemshangaza Simoni atakushangaza na wewe
Yesu atakuonyesha kwamba mifumo yako ya imani imekuwekea ukuta
Imekuwekea ukomo
Kuosha nyavu kulimaanisha kwamba hawawezi kuendelea kabisa
KUliamaanisha hawana matumaini tena
Umeona vyema kusali tu, umeona uishi tu kuliko kuendelea kuumia na kuchoka
Umeridhika na mashua isiyo na samaki jambo ambalo kwa simoni lilimaanisha hakuna biashara siku hiyo
Hakuna kipato siku hiyo
Unapopitia hali hiyo popote ulipo katika shughuli zako za kujipatia riziki unafika hatua ya kujidanganya ili ujifariji kwa kusema haukuwa mpango wa Mungu
Usihofu, hata Simoni alifikiri hivyohivyo ndio maana hakuonekana kupambana
Hakuonekana ana huzuni
Hakuana ni jambo baya, maana limezoeleka maishani mwake
Simoni alikuwa anaosha nyavu:
Kuosha nyavu kuna maanisha hakuna atakayekupenda
Kuosha nyavu kunamaanisha huwezi kuongeza elimu tena
Kunamaanisha umeamua kwamba huwezi kwenda mbele
Kuosha nyavu ni kuzikatia tamaa ndoto zako na kudhani kwamba jitihada zako zote zilikuwa kwa ajili ya usiku
Na kwa vile hakuitokea kama alivyodhani, kama alivyozoea
Aliacha kuvua akawaanaosha nyavu
Yuko hai lakini ameacha
Anapumua lakin ameacha
Utashangazwa kukutana na watu wanaopumua alakini wamekufa
Wana make up, wamevaa suti, wavaa vizuri, lakini wameacha
Wanakuja kanisani lakini wameacha
Wameacha!
Wanapeana maua lakini wameacha
Wanapika chakula lakini wameacha
Watu wanaweza kuacha huku unaowaona sebuleni, huku unawaona kanisani
Huku unawaona nyumbani
Watu wanaacha huku wanaendelea kutoa sadaka
Simoni aliacha kuvua lakini alitoa mashua yake
Kuacha ni kujiondoa bila kuondoka
Moyo wa Petro ulikuwa umevunjika na alikuwa anaosha nyavu
Aliacha lakini bado alikuwa anafanya usafi kanisani
Bado alikuwa anapamba kanisani
YESU ANAVURUGA MIFUMO YA IMANI YA PETRO
Hata kama Petro alitaka aendelee kuosha nyavu zake Yesu alitaka asiendelee kuosha nyavu
Lile linalokufanya uwe na amani nalo ndilo linalokufanya uwe umeacha hata kama tunakuona
Kuna watu wameacha kazi hata kama wako kwenye vituo vya kazi
Kwa sababu hawajafikia malengo
Wanapukuta meza lakini wameacha
Wanafuta madirisha lakini wameacha
Wanaenda kazini lakini wameacha
Kuna watu wameacha uinjilisti hata kama unawaona na Biblia
Wanachofanya ni kupukuta Biblia
Ni kusafisha kanisa
Wamekata tamaa baada ya kufanya kazi bila kupata samaki
Samaki ndio malengo! Samaki ni lengo la uinjilisti
Umeshindwa kwenda mbali peke yako
HUjapata samaki lakini wapo
Yesu anayetosha kwenye pochi ni tofautina Yesu wa kilindini
Tuna Yesu ambaye ni mvunja nira na kongwa
Yesu anakuja nyumbani kwako
Anakuja kwenye uchumi wako
Anakuja kwenye elimu yako
Anakuja maishani mwako
Anataka kutumia mashua yako ili iwe mimbari yake kuwahubiria watu
Baada ya hapo kila jambo ulilodhani limefika mwisho litaanza upya
Mungu anataka ujue kwamba mashua ni maisha yako,
Mashua ni biashara yako
Mashua ni elimu yako
Mashua ni familia yako
Una mashua ambayo ina ukubwa uliosababishwa na mazoea, ukimpa Yesu aitumie itajaa samaki
KIPELEKE MBALI KIDOGO NA PWANI
Kisiwe kilipokuwa
Kisiwe mbali na watu lakini kisiwe mahali walipo watu
Yesu hakuingia kwenye mashua na kuanza kuongea na watu, alitaka kuwe na juhudi ya Petro
Sio tu Yesu anakuja kwako na kuingia kwenye maisha yako na kuanza kuyatumia
Sio anaingia tu kwenye biashara yako na kuanza kuitumia
Sio anaingia tu kwenye utumishi wako na kuanza kuugeuza kuwa madhabahu
Bali anataka uyasogeze maisha yako mahali ambapo patafaa yeye kuongea na watu
Kuna jitihada inahitajika kabla maisha yako hayajawa madhabahu,
Kabla miili yetu haijawa dhabihu kuna jitihadi ya positioning
Jambo ninaloliona hapola uhakika ni kwamba Yesu anaweza kuingia maishani mwako na ukawa naye
Lakini kama unataka Yesu aongee na watu ni lazima ufanye alichofanya Petro-positioning
Mwanzo wa uamusho kwa Petro ni pale anapoacha kuosha nyavu na kurudi kwenye mashua ili aisogeze ili Yesu aitumie
HIli ndilo lengo la mimi kukualika ili uache kuosha nyavu, urudi mashuani, uendeshe sio kwenda kuvua samaki wa biashara bali Yesu aitumie mashua yako kwa namna ambayo sio malengo ya mashua yako
Sio malengo ya waliotengeneza mashua
Akutumie nje ya malengo ya wazazi wako
Nje ya malengo yako
Akutumie kwa malengo yake huku ukiwa umekosa malengo yako
Haikuwa rahisi!
Wengine mngesema mashua nimekupa isogze mwenyewe mimi ni mechoka
Usinisumbue sijalala usiku kucha
Ilihitaji utii nyakati ngumu
Ilihitaji utii nyakati una njaa hujala
Ilihitaji utii nyakati ambazo watoto wako walitegemea urudi na samaki na hujarudi na Yesu anataka akutumie kuisogeza mashua
Kwani ungekubali kuisogeza mashua kwa ajili ya mtu usiyemjua na hajakwambia anataka aitumie kwa ajili gani
Lakini kwa nini aliichagua mashua ya Petro?
Hata mimi ningejiuliza hilo swali kabla sijaamua kukataa aua kuisogeza mashua
Petro anadondosha nyavu zake na kwenda kuendesha mashua kwenda anakotaka Yesu
Toa ulicho nacho kwa ajili ya Yesu, maisha yako, ajira yako, mali zako, elimu yako, muda wako, ujuzi wako, nguvu zako
Alichofanya Petro ni Uamusho!
Acha kujilaumu
Acha kuongelea ulivyoshindwa
Acha kuongelea ulivyopata hasara
Acha kuongelea nguvu uliyotumia ambayo haikukupa chochote
Unapoosha nyavu unawaza ulivyoshindwa sio unavyoweza kupata
Hayo yamepita
“Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kkiumbe kipya…”
Huwezi kubadilisha lililotokea
Yaliyopita yamepita
Usisishi leo huku unafanya mazoezi jana
Jana yako isiibe leo yako
“Bwana tumefanya kazi usiku kucha lakini hatukupata kitu”
Yesu anasema tweka kilindini Petro anazungumzia walichofanya usiku
Imani inamwambia ukikosa usiku mchana huwezi kupata.
Yesu anasema, Petro anasema
Yesu anasema, Mazoea yanasema
Yesu anasema, kukata tamaa kunasema
Ni kama anasema haiwezekani
Oh Haleluya! Naona jambo lingine hapa,
Kilindini ndiko mahali ambako wavuvi wengi hawaendi lakini ndiko samaki wanakokuwa nyakati za mchana
Kilindini mashua inazama
Kilindini hakujazoeleka
Kilindini kuna samaki
Mwambie jirani yako, utakosa samaki kwote lakin Yesu anasema sio kilindini
Baada ya biashara ya Petro kuwa madhabahu
Baada ya maisha ya Petro kuwa madhabahu
Baada ya uchumi wa Petro kuwa madhabahu
Na umati ukiwa ufukweni, Yesu alihubiri na watu waliona heri kuzimia na njaa kuliko kukosa kumsiliza Yesu
Mwite leo aketi maishani mwako
Alipomaliza kuongea na watu, na hapa hatujaambiwa aliongea nini na watu kwa sababu nguvu ya aya ipo kwenye matemdo yaliyotokea
Alimwambia simoni ” Tweka kilindini”, Shushueni nyavu
Nyavu zilizooshwa?
“Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mabamo yasiyoonekana” Waebrania 11:1
Kurudisha na kuzishusha nyavu kilindidni kulimaanisha zitahitaji kuoshwa tena.
Ilihitaji imani!
“Lakini Pasipo hiyo imani haiwezekani kumpendeza…”
Ilihitaji utii
“Tweka kilindini”
Bado hujaelewa,
Yesu anasema ondoka kwenye maji machache zamisha nyavu kwenye maji mengi
Sema “kilindini”
Mwambie ulipo hapana kina cha kutosha kupata samaki. Maisha yako yamezoea maji madogo tweka kilindini
Ukitaka kupata maarifa ya Mungu ondoka kwenye maji madogo tweka kilindini
Kinachofanya uwe hivyo ulivyo sio bahari kutokuwa na samaki bali ni wewe kutompa Yesu maisha yako ili akwambie walipo samaki
NI kwa sababu hujaenda kwa kina
Umetumia nguvu nyingi, umetumia mali nyingi, umetumia muda mwingi kwa akili ya mazoea
Jiandae kuona anachoweza kukupa Yesu
Shetani alilenga kukutesa
Shetani alilenga usihindwe kutunza watoto wako
Shetania lilenga kukuhuzunisha
Pengine Petro alihitaji samaki siku ile kuliko nyingine yoyote kwa ajili ya familia yake
Ndio wakati ambao alikosa samaki
Hata kama sina hakika
Hata kama sijawahi kwenda
Hata kama kunatisha
Hata kama nyavu zitachafuka
“kwa neno lako Nitazishusha nyavu”
Warumi 10:17 “imani chanzo chake ni kusikia na Kusikia huja kwa neno la Kristo”
Luka 6:46-49
Tweka kilindini!
Kilindini ni kina kirefu
Lazima useme nimechoka kuishi ndani mipaka, ndani ya vizuizi sasa najianda kwenda kwenye kina
Naendaa kuzishusha nyavu
Naenda kwenye viwango vipya
Hujui kwamba sababu ya Mungu kukupa ulivyo navyo ikiwa ni pamoja maisha yako ni kwa sababu anataka viwe jukwaa la injili
Heshima ya maisha yako iwe jukwaa la injili na sasa unahangaika na matatizo na matatizo hayako kwenye kile unachofanya
Matatizo yako ndani yako
Ukimsikiliza Yesu, Ukimpa YEsu mashua yako aitumie
Kila kitu kitabadilika
Kila kitu kwenye maisha kitabadilika
Tweka kilindini wakati watu wanadhani utaosha nyavu
Wanapodhani utaacha tweka kilidini
Wanapodhani utajiua tweka kilindini
Wanapodhani watoto wako watakufaa njaa tweka kilindini
Mwambie jirani “nashusha nyavu kilindini”
Usipozisha nyavu kilindi huwezi kupata samaki
Ukiogopa kufa kilindini huwezi kupata samaki
Twende kilindini au ubaki ufukweni
Twende kilindin au uendelee kuosha nyavu huku umeacha
Wengine wanasema sijawahi kwenda kilindini, lakini hilo haliondoi kilindi kuwa na samaki unaowakosa kwenye maji madogo
Yesu amekupa kibali cha kwenda kilindini, nenda samaki wapo
Kilindini kwako ni wapi?
Labda ni kijiji fulani, labda ni mkoa fulani, labda ni tv fulani, labda ni redio fulani, labda ni ofisi fulani, labda ni chuo fulani, labda ni shule fulani
Sijui Yesu anakutuma kwenda wapi lakini ninachojua kilindini kuna samaki
Kwa kawaida nyakati za mchana huwezi kuvua lakini Yesu akisema nitaenda kilindini
Mazoea yanasema lile ni kabila gumu lakini Yesu akisema nitaenda
Mazoea yanasema kule ni ghrama kuishina familia yangu lakin Yesu akisema nitazishusha nyavu
Mazoea yanasema kule sijaozoea laini Yesu akisema, nitaenda
Moyo wangu unasema siwezi lakini kwa neno la Bwana nitaizishusha nyavu
Shetani anapokukatisha tamaa kwamba haiwezekani,
Umepodhani majira na nyakati zimepita
Yesu anasema samaki wapo
Unajiuliza kwanini, unajiuliza inawezekanaje?
Ni kwa sababu simoni anamiliki mtumbwi lakini Yesu anamiliki samaki na anajua walipo
Simoni ana mtumbwi lakin Mungu ana bahari
Yesu anajua walipo samaki unaotafuta usiku kucha
Wakati ambao wenzio wanaosha nyavu na wengine wamelala vimvurini ndio wakati wa kumsikiliza Yesu anataka kukutuma wapi
Wengi wanaangalia wasiofanya kazi, wanaolala, wanaoosha nyavu na wao wanaosha nyavu
Vunja sheria ya mazoea!
Sheria inasema samaki wanapatikana usiku Yesu anasema usiku ni wakati wa kazi za shetani
Shetani anajua unajua kwamba samaki wapo usiku na hivyo anapiga usiku
Yesu anasema samaki sio tu wapo mchana lakini wapo kilindini
HUjachelewa kwend akuanzisha kusanyiko
HUjachelewa kufungua huduma
Unachochelewa ni kufika kilndini
HUjachelewa kuanzisha biashara bali biashara yako imeshusha nyavu kilindini?
HUjachelewa kuanza maisha, lakini je uko tayari kwenda na Neno la Bwana!
Jiandae kwenda kwenye kipenyo kipya
Kazi yako ni kushusha nyavu, kazi ya Mungu kukupa samaki
Kazi yako ni kumpa Mungu ulicho nacho, Kazi ya Mungu ni kukwambia kwa kwenda kuzindua upya maisha yako
Navunja vizuizi na mipaka uliwekewa maishani mwako
Navunja mipaka iliyokubakisha ulipo
Najunja vizuizi vinavyosimama kati yako na Neno la Bwana
Nafungua malango yaliyofungwa maishani mwako
Mipaka imezoeleka mpaka imekuwa maisha yako
Imezoeleka mpaka imekuwa wewe
Hadi umejikuta wewe ndio mipaka yenyewe
Hadi unaitetea
Umekata tama kiasi cha kutumia muda wako kuosha nyavu
Umeacha kuvua unaosha nyavu, nakwambia acha kuosha nyavu anza kuvua
Mungu anataka usiache ulichoacha
Mungu anasema acha unakataa kuacha, ulichochelewa kuacha
Mungu anasema rudi ukavue
Uende unakosita kwenda
Uende unakoogopa kwenda
Huu sio wakati wa kuosha nyavu
Huu ni wakati wa kuzishusha nyavu
MASHUA YA PETRO ILILINGANA NA MAZOEA
Nimewahi kuona majengo yanayotosha watu 15. Wengine wanasema kubwa la nini?
Walipozishusha nyavu, samaki walikuwa wengine hata nyavu zikataka kukatika
Walipoomba msaada kwa wengine mashua zao zikataka kuzama
Watu wanawaza na kutenda sawasawa na mazingira. Petro na wengine walikuwa na nyavu zinazotosha samaki walizozoea
Nyavu ulizonazo hazitatosha na jambo pekee unalopaswa kuomba kwa Mungu ni kuomba akili. Kuomba mabadiliko ya akili
Hili jambo lenye uhusiano na nyavu,
Wanapokutana na Yesu alikuwa wanaosha nyavu
Walipoingia kwenye mashua hawakukagua ukubwa na uimara wa nyavu
Kwanini Petro hakushusha nyavu imara
Kwa nini hakushusha nyavu kubwa
Kuridhika kwako kunatangulia mbele ya Neno la Bwana
Mazoea yako yanakuwa mbele ya ahadi za Mungu
Petro hakujua kama nyavu zitatka kukatika
Hakujua kwamba atahitaji msaada wa wengine
Kwa sababu hajawahi kufikiri hivyo
Aliziamini nyavu kuliko kuamini Neno la Bwana
Hata kama alisema kwa Neno lako nitaenda
Alijua suala ni kushusha nyavu
Alijua kushusha nyavu kilindini ni kushusha nyavu
Kushusha nyavu kilindini kumaanisha kukagua nyavu ulizonazo
Kulimaanisha kutathimini rasilimali alizonazo kama zinaendana na kilindini
Alitumia nyavu za maji madogo kwenda kilindini
Shusha nyavu!!!
Kilindini kuna samaki wengi sana wanaosubiri utii neno la Bwana
Kilindini ni tofauti na ulipozoea na kuzoeleka
Utii ndio utakaovunja mipaka
Mipaka ya mafanikio ya Petro haikuwa baharini
Mipaka ilikuwa kwenye nyavu na mashua
Hakuna anayeenda kuvua na amshua ambayo anategemea umwombe akusaidie kubebea samaki zako
Kila anayeenda kuvuaa anaenda na chombo kinachotosha na anaenda nyavu inayotosha
Maisha ya Petro yalitosheka na samaki walioendana na nyavu alizokuwa nazo
Hatuwezi kusema Petro hakumtii neno la Bwana! Angalau anatofautiana na wengi wetu
Alitoa mashua itumiwe na Yesu
Alikubali kumpeleka Yesu mahali pa kuhubiria
Warumi 10:14-15
ìWataendaje wasipopelekwa?
Angalau Petro alihatarisha maisha yake (mashua) kwenda sehemu ambayo hajawi kwenda na angezama pia
Lakini alienda
Angalau alikuwa na imani ya kubeba nyavu akiamini atavua
Lakini anafanana na wengi wetu hasa watumishi wa Mungu kwa kwenda kilindini na tabia(nyavu) za maji madogo
Nyavu ndizo hunasa samaki na tabia zetu ndizo hunasa watu waje kwa Kristo
Mungu amehifadhi samaki wengi kwa ajili yako kama uko tayari kwenda
Mifano ya Mungu Warumi 11:4
ìKwanza utanulizeni ufalme wa Mungu na haki yakeî
Wengi hatuamini hii aya hata kama tunaisoma ndio maana nimesema Kuna uwezekano ukawa huamini unachoamini
ìNa hayo yote mtazidishiwaî
Kuzidishiwa kwa namna ya kukatika nyavu
Kuzidishiwa kwa namna ambayo utahitaji msaada
Mtangulize Mungu katika uchumi wako
Mtangulize Mungu katika kazi zako
Mtangulize Mungu katika kilimo chako
Mtangulize Mungu katika biashara zako
Ukifanya hivyo tii neno la kwenda kilindini
Utakata nyavu
Luka 6:38
Petro na wenzake mashua na nyavu zao hazikutosha
Na Mungu ameniambia nikwambie kwamba samaki hawakuisha kilindini ila Petro mahitaji yake hayakufanana na mashua na nyavu alizo nazo. Jambo hili lilimfanya aache samaki ambao angewahitaji kesho
Kuwa makini na kibebeo cha majibu ya maombi unayomwomba Mungu
Mahali huduma inaenda itahitaji wasaidizi
Mahali maisha yanaenda utahitaji wasaidizi
Mahali biashara yako inaenda utahtaji wasaidizi
Lakini kwanza ufalme wa Mungu kisha Tii na hayo yote Ö..
Unahitaji mashirikiano
Kwa sasa unafanya mwenyewe kila kitu kwa sababu hujatweka kilindini
Kila anayechukua neno hili popote ulipo unapaswa kuwa na mpango mkakati wa kuhimili uzito kiwango kinachozidi kiwango ulicho nacho sasa
Utahitaji vitendea kazi
Nawaona wengine wakiwa wainjilisti wa mikoa, wainjilisti wa Taifa, Wainjilisti wa kimataifa
Nawaona wengine wakiwa wafanyabiasha wa kimataifa
Tweka kilindini
Lakini unahitaji passpot kuliko unavyohitaji Nida
Matokeo ya kilindini huwezi kuyabeba kama ulivyozoea kwa sababu yapo kinyume na mazoea na mifumo ya imani
Kwa sababu kilindini kunazidi mifumo utahitaji kuandaa mifumo
Petro alivua samaki wangapi?
Aliacha samaki wangapi?
Lakini Petro alikosa samaki wangapi kabla ya pale
Samaki hawa wote walikuwa wanaishi palepale Genezareti
Walesamaki hawakuumbwa siku ileile
Walikuwepo siku zote
Hivi unajua umekosa mangapia miaka yote hii kwa kushindwa kumpa Mungu maisha yako ayatumie
Kwa kushindwa kumepeleka Yesu akahubiri vijiji mbalimbali
Kwa kushindwa kutii?
Ni kweli unamwini Mungu
Ni kweli umebatizwa
Ni kweli ni kiongozi kanisani kwenu
Lakini inawezekana huamini
ìBwana nisaide kutokuamini kwanguî
Unapoosha nyavu, mashua hujaiosha-Mpe Yesu itafaa tena
Unapoosha nyavu unadhani ndio basi
Kuna samaki wengi kilindini
Wengine mali mlizonazo zinawazuia kwenda kilindini
Ndugu mlionao mmewazoea sana hata hamuendi kilindini
Nyumba uliyojenga hutaki kuiacha ili ukahubiri vijijini
Watoto ulionao wamekuwa kizuizi cha kwenda na hivyo upande wa pili wamekuwa kizuizi cha Baraka zako
Samaki wapo kilindini
Mungu anataka kukuonyesha kwamba yapo mengi usiyoyajua
Mwambie jirani nimepewa kibali kwenda kilindini!
Mshauri jirani yako abadilishe nyavu na mashua
Kilindini kuna samaki
Una kibali cha kuvua samaki mchana
Una kibali ambacho wengine hawana
Kibali kinakufanya uvue samaki wakati usio kufaa maana wakati unaokufaa ni usiku
Anachotaka kukupa Mungu kwa kawaida hakikupaswa wakati huu wa huduma yako, wakati huu wa umri wako
Ukiachana na mapokeo, Mungu atakufungua
Onyo ni kwamba mapokeo na mazoea yatakufanya ukose samaki ambao Mungu amekuandalia
Umeitwa na Mungu uende kilindini na sio kwenye maji ya ugoko
Huwezi kupata maarifa ya kina ya neno la Mungu kwenye maji madogo
Huwezi kupata mafanikio kwenye maji madogo
Huwezi kuvua samaki wa kukutosha kwenye maji madogo
ILI UPOKEE ALIKUANDALIA MUNGU UKUBALI HASARA
Nyavu zilitaka kukatika-usidhani hazikuonyesha nyufa
Mashua zilitaka kuzama-usidhani hazikuanza kuzama
ìatakayepoteza maisha atayaonaî
Wafil. 3:7-9
Ukubali mabadiliko maishani mwako
Kuna mambo yatavunjika
Kuna urafiki utavunjika kutoka na uzito wa utukufu wa Mungu maishani mwako
Utalazimika kuvunja imani ulizozoea
Hii ni zaid ya samaki
Biblia ya King James inasema walivua ìmultitudes of fishî. Yaani lundo la samaki mst. 9
Nasema ni zaidi ya samaki kwa sababu jicho la ndani Linaona mambo mawili
1. Biashara-Uchumi-mafanikio-rasilimali-kipato
Biashara ya Petro inaenda mbali na upeo wa kibindamu na mazoea
Kujaza mashua yake
Kujaza mashua za wenzake hadi kila kiti chenye uhusiano na Petro kilipojaa.
2. Uinjilisti
Kwa hiyo unaposoma hapo usisome habari ya samaki tu bali kuna biashara na uinjilisti
Walipoegesha vyombo vyao Biblia inasema walimfuata Luka 5:10-11
Mathayo 4:16
PETRO KUKUTANA NA YESU HAIKUWA MATOKEO YA UTAKATIFU WAKE
Luka 5:8
ìondoka kwangu maana mimi ni mwenye dhambiî
Samaki hawakuwa thawabu ya utakatifu wake bali samaki walikuwa thawabu ya utii wake
Sema utii unalipa!
Alitoa mashua
Alimpeleka YEsu
Alimtii Yesu
ìKwa neno lako nitazishusha nyavuî
Yesu alimbariki Petro na biashara yake na akamwahidi kumbariki zaidi na zaidi
ìTangu sasa utakuwa unavua watuî
Ngoja nikupe siri iliyoko hapa
Mazungumzo haya yanafanyika mwanzoni mwa huduma ya Bwana Yesu na Mwishoni mwa huduma ya Bwana Yesu
Na nyakati zote mbili Petro anakutwa amekata tama
Nyakati zote mbili Petro anatumwa kuvua samaki
Na nyakati zote mbili anakutwa hajapata kiti
Mwishoni mwa huduma ya Yesu, Petro anarudi kuvua samaki kwa sababu Yesu amesulubiwa na ameshakufa
Yohana 21:1-12
Yesu alipokuwa akitembea pembezoni mwa bahari baada ya kufufuka kwake
Na mazungumzo yanafanana kwa kiasi kikubwa
ìWalimwambia tumefanya kazi usiku kucha lakini hatujapata kituî
Yesu aliwaambia tupeni jarife upande wa kulia wa mashua
Kutokana na wingi wa samaki waliopata ulimsaidia Petro kukumbuka
Tukio la kwanza
Ni kama alifika duara ya maisha yake ilipoanzia
Lakini kwa sasa haikuwa kilindini
Kumwelewa Yesu maishani mwako kunakusaidia kujitambua maishani mwako
Wengine wanamwelewa Yesu lakini hawajielewi wenyewe
Wengine wanawaelewa wengine lakin hawajielewi wengine
Safari hii Petro hakungoja afike na samaki ufukweni
Alisema hatafanya makosa aliyofanya mara ya kwanza
Alijisemea moyoni ìhaa kama amenibariki kwa samaki, hili sio jambo la samakiî Ni jambo la uinjilisti
Hilo sio jambo la uchumi tena bali ni la uinjilisti maishani mwako
Ni jambo la kupata kifungua kinywa ukahubiri ni jambo la Bwana!
Petro akaruka na kuanza kuogelea kwenda kwa Yesu
Kuna wakati inabidi uache biashara unapofika muda wa Bwana
Kwana wakati inabidi ufunge ofisi unapofika muda wa Bwana
Kuna wakati inabidi uondoke numbani unapofika muda wa Bwana
Safari hii aliacha mtumbwi ukiwa umekwama na samaki 153
Najiuliza ile mashua ilikuwa ni nyingine au ni ile ile aliyokuwa nayo mwanzo?
Safari hii hakupanda mashua
Watu waliokata tama wana kawaida kurudia walichokuwa wanafanya mwanzo
Waliokata tama wana kawaida kuwarudia marafiki wa zamani
Tusiache kuwatembelea na kuwakumbusha
Tusiache kuwapenda
Biblia inasema safari hii Petro alikuwa uchi
UKIENDA KWA YESU ULICHOACHA UNAPATA KWA YESU
Alipofika alikuta Yesu anabanika samaki-Wakati wanaenda kuvua samaki Yesu alipata wapi samaki?
Petro aliachana na samaki wa kwenye mashua lakini hakukosa samaki
Faida ya kwenda kwa Yesu
Faida ya kumkimbilia Yesu
Unaacha samaki wabichi unakutana na samaki aliyeiva! Haleluya!
Unapoacha samaki wabichi ni lazima usijua kama kuna samaki walioiva ufukweni ili iwe thawabu ya imani
Petro safari hii alipata thawabu ya imani
Zaburi 23:5
ìBwana anannidalia meza mbele ya watesi wanguî
Utatembea ndani ya Baraka zilizoandaliwa na Mungu kwa ajili yako
Yesu alijua Petro atafanya maamuzi sahihi ndio maana akawa anaoka samaki wakati Petro anaogelea
Fanya maamuzi sahihi leo
Mungu anakuandalia kifungua kinywa, chukua hatua!
Vunja mipaka
Vunja mapokeo
Kwa mara nyingine Petro anahatarisha uhai wake
Mara ya kwanza alihatarisha kwa ajili ya samaki na sasa anahatarisha kwa ajili ya Yesu
Anaogelea akiwa uchi
Mwambie jirani yako ìutapata mengiî Marko 10:28-52
Baada ya siku ile hatumwoni Petro akiwa na mashua kwa ajili ya samaki
Petro alikuwa ameliewa kusudi kuu ambapo mashua ilikuwa ni mafunzoni tu
Kama unanielewa, ni hivi;
Usiomboleze kwa ajili ya mambo uliyopoteza
Chochote unachowekeza kwa Mungu,kipawa, mali, muda havijaiva, Mungu anakuandalia samaki waliookwa ufukweni
Ninakuombea kwa sababu najua adui alikuwa anaogopa sana kwa wewe kupatana neno hili
Anaogopa kwa sababu Mungu anaenda kukufungua
Alikuzuia kwa njia nyingi
Alikuwekea majaribu ili usifike kilindini
Ili usifike ufukweni
Anakuzuia usifanye kazi ya Mungu ili urudi kwenya uliyozaliwa nayo
Na hiy o ndiyo njia pekee ya kuzuia utii
Utii ni kufanya niliyoagizwa na Bwana
Mungu amekuandalia Baraka, kama unadhani hili ni somo tu ni shauri yako lakini wengine wanachukua kama ujumbe wa Bwana maishani mwao
Mungu anataka kuyatumia maisha yako kama jukwaa
Tatizo la kwanza hatuko tayari maisha yetu yawe jukwaa
Pili hata tunapokuwa tayari nyavu zetu ni ndogo kuliko ufalme wa Mungu
Ni sadaka gani unaweza kumpa Mungu zaidi ya maisha yako?
Ni alama gani unaweza kuiweka kwenye kanisa kama sio maisha yako na mali zako
Baadhi yenu mna moyo kuweka alama, wa kutoa sadaka lakini hamkuwahi kubahatika hata kuwasaidia wazazi wenu hadi wameondoka duniani na unaomba wangekuwepo ingeweka alama maishani mwao ingawa sio kuwalipa
Hapa kuna Mungu ambaye unamhitaji kuliko anavyokuhitaji lakini anakupenda kuliko unavyompenda
Mungu amekupa fursa ya kumpa maisha yako
Fungua mipaka iliyofungwa maishani mwako Katika jina la Yesu Kristo!
Navunja ukomo uliowekewa!
Endelea kuomba, Mwambie Mungu akuonyesha maeneo yaliyofungwa maishani mwako
Chuki, wivu, uadui vinaua kesho yako
Jinsi unavyojidharau unaua kesho yako
Jinsi usivyojiamini unasababisha watu wasikuamini
Kama sikwambii haya kwa sababu niko hapa basin i kwa sabab Mungu ameniambia nikwambie
Kama unaweza kulipokea neno hili sasa lipokee
Wengine wamelisikia lakini hawajasikiliza
Wamelitazama miaka mingi lakini hawaliona
Lakini kama umeliskia na kuliona ni kwa sababu tu roho amefungua masikio na moyo wako ulipokee
Na hiyo ni Baraka
Tenda sasa sawa sawa na neno hili
Uwe tayari kumpa Mungu maisha yako na mali zako
Ili ninapoomba niifunike sadaka yako
Ni muhimu sana ili usirudi kuvua samaki tena
Ni muhimu ili usirudie kuwa mwongo mwongo tena
Ni muimu ili usirudie kuwa mjanjamjanja tena
Kwa sababu Mungu atakuvusha kutoka imani hata imani
Kutoka utukufu hadi utukufu
Na ataendelea kufanya mambo makuu ndani yako na kukupeleka katika viwango vya juu katika kumjua kwa ajili ya kusudi lake mwenyewe
Mwambie jirani yako
ìMungu hajaishia hapa, hajamalizana na wewe bado
Acha kuosha nyavuî
Yesu atageuza maishua yako kuwa jukwaa
Na hiyo itabadilisha mweleko wa maisha yako
Akikaa kwenye mashua yako kila kitu kitabadilikaî
Inua mikono niombe na wewe
ìAsante Yesu, mimi mtumwa tu bali wewe ndiye uliye na kusudi la maisha yangu
Kusudi la kuzaliwa kwangu, kusudi la kuumbwa kwangu
Kusudi la kuokoka kwangu
Nakupa kila eneo la maisha yangu
Siwezi kufungua mipaka bila wewe kwa sababu wewe ndiye ufunguo
Naomba unifungue niishi maisha uliyokusudia niishi
Nisaidie nitimize kusudi lako maishani mwangu
Naminiuone utukufu wako na sio heshima yangu
Ili ulimwengu ujue kwamba wewe ni baba yetu
Katika Jina la Yesu Kristo, Amen!