WAKATI NI KILA KITU
Mathayo 13:24-30
Nilianza kuwaza kuwa na shule ya Biblia miaka mingi sana lakini Sidhani kama nilijua kwamba mambo mazuri huhitaji muda
Nilipokuwa mdogo sikuwa na subira lakini sasa naelewa mambo mazuri yanahitaji muda
Mambo madogo madogo kama chakula huhitaji maandalizi na maandalizi yanahitaji muda
Siku hizi watu hawana muda wa kupika lakini wanakula
Hata watu wa kufanya nao kazi unahitaji muda kuwapata
Mambo mazuri huhitaji muda
Una pesa lakini huna hekima sio muda utabaki na hela bila watu
Kukua kunahusiana na mafunzo unayojifunza unapopanda juu
Kuna mambo unajifunza huku unapambana na kuna vitu unajifunza wakati unapitia majaribu
Inachukua muda kufanya vyema na kwa hakika inachukua muda kuwa vizuri.
Muhubiri 3:1-2
Kila jambo lina wakati
Kila jambo lina majira
Kila kusudi lina wakati; Unapokuwa na kusudi, unajua wakati wa hilo kusudi?
Ni lazima tuelewe kwamba hata watu wapo ambao ni kwa ajili ya wakati na kusudi
Wengine ni kwa ajili ya majira Fulani yamaisha yako
Fursa fulani ni za majira fulani
Kama vile majira na nyakati zibadilikavyo ndivyo tunatakiwa kujua kwamba majira na maisha hubadilika na yanapobadilika usifikirie kwamba Baraka zimeisha
Baraka hazijakoma ila ni majira yamebadilika
Nikipata muda nitazungumzia ulinganifu wa majira ya kuzaliwa na msjira kufa
Wakati wa kupanda na wakati wa kungíoa kilichokuwa kimepandwa
Je unaelewa utofauti wa maisha yako?
Je maisha yako yana majira na nyakati?
Utofauti wa kujua majira na nyakati za kupanda na kungíoa
Umewahi kumwomba Mungu ili akupe kujua wakati na majira sio ya mwaka bali majira na nyakati za maisha yako?
Au dhamira yako ni kutunza yaliyopandwa?
Dhamira yako ni kutunza uliyoyazoea na huwezi kuupa mkono wa kwa heri Wakati na majira uliyokuwa nayo
Unatunza yaliyopandwa hadi yakufie
Ni lazima uwe na roho ya kuachilia bila kugombana ili kukumbati majira ambayo Mungu anataka kuyaong’oa
1Kor. 13:11-12
Majira ya utoto
Kama bado unawaza kama ulivyokuwa unawaza wakati una miaka 10, habari mbaya ni kwamba una ulemavu rohoni na ulemavu huo unayazuia mawazo kuongezeka na yanabaki kwenye kipimo kile kile
Unajiuliza inawezekanaje? Ni kwasababu kama Unangíangíania majira na nyakati unayachelewesha majira mapya maishani mwako
Kuishi kwenye majira na nyakati zako ni jambo muhimu sana
Wakati ni kila kitu!
Sema, Mungu nifundishe nijue nyakati na majira yangu
Unaweza kuwa sahihi unachoongea lakini ukawa sio wakati sahihi wa kusema
Taarifa zingine zitasababisha nyumba ianguke
Mtoto ajisikie kunyanyaswa
Wakati ni kila kitu Waefeso 4:17
Ni lazima ufanye kila jambo kwa wakati na majira yake vinginevyo hutakuwa na matokeo unayoyatamani
Je unafahamu saa hizi ni majira gani kwenye maisha yako?
Kuna saa maishani mwako inayosoma majira na nyakati za maisha yako
Nina saa mkononi inayoniwezesha kujua ni saa ngapi lakini unajua ni saa ngapi maishani mwako
Katika utumishi wako?
Katika Ukristo wako?
Je ni wakati wa kungíoa?
Je ni wakati wa kupanda?
Umuhimu wa maswali haya ni kwamba unaweza tu kuzaa matunda ndani ya majira yako
Kanisa linaweza kuzaa kama lipo ndani ya nyakati na majira
Cha muhimu hapo ni kwamba hakuna matunda yanayopatikana nje ya majira na nyakati
Ni lazima ujue nyakati za kungíangíania na nyakati za kukunja
Bila kujali ni aina gani ya mti uko juu ya ardhi, kunakuwa na mizizi iliyoshikana ardhini
Hata magugu yana mizizi lakini mizizi ya magugu ni mikubwa kuliko mizizi ya ngano
Kabla sijaingia kiundani nataka ujiulize kwa nini unajifunza somo hili hata kama umesoma hii aya siku zote
-Je hii nafasi inamaana gani kwangu?
-Mungu anakukumbusha kwamba uko katika majira gani?
Waebrania 5:11-12
Wakati wa kukua
Ukiheshimu Wakati na majira yako utaheshimu saa yako ya mkononi
Usipoheshimu hutaheshimiwa, hutaheshimika,hutafanikiwa kiuchumi, hutakuwa na nguvu
Ni wale tu masikini ndio wanaokuwa masikini wasipoanza kuheshimu majira na nyakati za maisha yao
Hao ndio ambao wakati wanaokuwa nao ni ule wakifumbua macho kutoka usingizini
Sasa turudie kusoma Mathayo 13:24-30
Walipolala
Adui ndipo alipopanda magugu- wakati Fulani nimekuwa nikihubiri kinyume na waliolala uzingizi hadi niligundua kwamba binadamu wote huwa tunalala usingizi
Ila ni jambo la hatari kulala usingizi nyakati ambazo sio majira ya kulala usingizi
Hata hivyo wengine wanalala
Hapa tunaona kwamba watumwa hawagundua asubuhi kulipokucha kwamba kuna mabadiliko shambani
Kuna nyakati na majira hutarajiwi kulala
ìOmbeni msije mkaingia majaribuniî Hata hivyo alikuta wamelala
Hata walipoamka asubuhi hawakugundua kama Adui alikuja pale achilia mbali kujua kama kuna mbegu za magugu zimepandwa
Adui alipanda wakati wamelala, na alipanda katika namna ambayo hata wakiamka wasigundue mabadiliko yoyote
1. KUPANDWA KWA HAKUONDOI KUPANDWA KWA MAJASUSI YA SHETANI
Matendo 20:28-32
Jambo jema huvutia baya
Mungu akiruhusu ngano kupandwa haimaanishi kwamba magugu yamezuiliwa
Kwa hiyo tunatakiwa kuzaa matunda mbele ya magugu
Kwako wewe unayesubiri magugu yaishe ndipo uzae matunda huchimbi hii aya kwa sababu aya hii inaonyesha kwamba hakutakuwa na siku maishani mwako ambapo hutakuwa na magugu
Ngano zilipandwa kwa malengo kwa maneno mengine ni kwamba ngano isingeota pale kama isingepandwa pale kwa sababu pale sio asili yake
Kuota ngano pale sio tokeo la hali ya asili ya hewa,udongo, mvua, jua. Kuna mtu aliamua kupanda mbegu ya ngano
Mvua haikuwa na mbegu ya ngano
Hewa haikuwa na mbegu ya ngano
Udongo haukuwa na mbegu ya ngano
Jua halikuwa na mbegu ya ngano
Tena,
Usifikiri magugu yalijiotea; Biblia inasema Adui alikuja kupanda magugu. Kwa hiyo hata magugu pale shambani hapakuwa asili yao
Kuna jitihada na timing ilifanyika
Mafanikio yanahitaji muda lakini yana mapambano
Ushindi unahitaji muda
Kupanda cheo kunahitaji muda
Uinjilisti, Ukristo, uongozi, ni jasho
Waliopanda ngano usidhani hawakutokwa jasho
Na aliyepanda magugu usidhani hakutokwa jasho
“Agriculture” ni intentional= Dhamira
Dhamira ya kupanda mbegu ni kupata ngano na dhamira kupata ngano ni kupata mkate
Mbegu—-Ngano—Mkate
Huwezi kupanda mbegu leo na kupata kula mkate jioni kwa sababu kila kitu kinahitaji muda. Kuna nyakati za kusubiri na majira ya kuvuna
Kuna nyakati za Subira ili kupata majira ya kuvuna
Kwa hiyo, kama unataka kuwa na matunda ni lazima ukue kwenda chini kwanza kisha juu
Wengi mnaacha kupanda kwa sababa kila ukiangalia nyumba huoni mbegu inayoota
Mbegu huota kuanzia chini na hukua chini kwanza. Mizizi haikui kupanda juu na majani hayatangulii mizizi
Ukisubiri Mbegu itabadilika kuwa ngano na kuwa mkate
Kuna kazi katikati ya kila hatua. Kupanda ngano ni kazi na kuvuna ni kazi
Huwezi kula vizuri kuliko unavyovuja jasho
Kuhusiana na Ahadi za Mungu (Mathayo 28:20) unapaswa kutambua kwamba unatarajiwa kutoa jasho, unatarajiwa kufanya kazi
Unapaswa kusaga ngano kwa sababu ngano sio mkate hadi usage
Mwambie jirani “ninatoka kwenye hatua ya mbegu ili niwe ngano na kisha niwe mkate”
Inawezakana sionekani kama mkate lakini niko kwenye hatua
Naelekea mahali fulani kwenye majira ya maisha yangu
Usinidharau kwa sababu sijawa mkate, inawezekana sipo kwenye hatua ya kuwa ngano,inawezekana niko kwenye hatua ya mbegu lakini jambo moja la ukweli ni kwamba natoka hatua moja kwenda nyingine kwenye hatima yangu
Ni lazima ukubali kuwa tofauti, Ni lazima ukubali kusemwa
Tatizo kubwa tulilonalo leo ni wasiwasi
Tunaogopa kutengwa kuliko tunavyoogopa kutozaa matunda
Unatumia muda mwingi kumwomba Mungu juu yale wanayokusema na Mungu anasema usipojikana mwenyewe hufai-Adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. Twende pointi namba mbili;
II. KILA PALIPO NA UWEZEKANO ZA MAVUNO ADUI ATAFUATILIA
Kupandwa ngano kulimfanya adui kuja kupanda magugu. Hakupanda magugu ili ngano zipandwe
Shetani alijua Mungu amekubariki, Kuzimu inajua Mungu anataka kukutumia, Kuzimu inajua Mungu ana kusudi na wewe ndio maana amekuwekea magugu maishani mwako
Mbegu za magugu zilipandwa kwa namna ambayo ni kama wapelelezi nyuma ya ngano na katikati ya ngano
Kila lililoharibika maishani mwako ilikuwa njia ya adui ili kukunasa
Sio kwa sababu ulikuwa na matunda bali kwa sababu ulikokuwa unaoenda ulikuwa unaelekea kuzaa matunda. Kwa hiyo alikuwahi
Alianza kuweka mifumo ardhini hata kabla mbegu ya ngano haijaota
Kabla huduma yako haijakua alihakikisha ameweka mifumo mahali ilipo mbegu ya huduma yako
Kabla hujawa mwaminifu 2Tim. 2:2
Adui aliweka miundombinu ili uwe na cha kupambana nacho
Kwa nini mambo ni magumu? Kwa nini napiga hatua mbili lakini narudi nyuma hatua kumi, Kwa nini kazi yangu ni ngumu sana wakati wengine huduma zao zinaenda kirahisi?
Ni kwa sababu Adui amepanda magugu katikati ya ngano
“walipolala” Adui akaja kupanda magugu
Kila palipo na ngano panakuwa na magugu
Kila palipo na mbegu za ngano adui anapanda mbegu za magugu
Na mbegu zote zilipandwa kwa matarajio
Hupambani na mapepo tu bali unapambana na mfumo wa mapepo uliowekwa na adui maishani mwako na sababu pekee ya kuwekwa mifumo hiyo maishani mwako ni kwa sababu wewe ni mbegu ya ngano
Wewe ni mbegu njema!
Shamba ni ulimwengu lakini mbegu zote sio za ulimwenguni. Mbegu unazopambana nazo sio za ulimwengu huu. Mifumo unayopambana nayo sio ya ulimwengu huu!
Waefeso 6:10-17
Shetani alipenya wakati wapandaji walipolala
Adui atasubiri mpaka asiwepo aliye macho kwenye familia yako, kwenye huduma, kanisani
Atasubiri kila mtu aondoke nyumani
Atasubiri mpaka uwe mpweke
Atasubiri mpaka wanaotarajiwa kuwa macho kwa ajili yako walale kwa sababu anatambua umuhimu wa wakati
“timing”
Kama alipannda wakati wamelala basi alipanda usiku, wakati wa giza
Sio tu mbegu alizopanda hazikuonekana, bali hata yeye hakuonekana anavyopanda
Wapandaji walipanda wakati kila mtu pamoja na adui wakiwa wanaona lakini adui alipanda wakati ambao wapandaji hawaoni na yeye mwenyewe hakuonekana. Alipanda gizani.
Na inawezekana wale wapandaji waliopanda mchana miongoni mwao adui alimtumia kupanda usiku-nawaza tu. Kwa sababu adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake
Giza la usiku lilimficha
Siwezi kuona aliyepanda magugu maishani mwangu lakini nayaona magugu
Siwezi kuona mbegu za adui lakini adui anaona mbegu zangu
Hila ya adui imeficha mbegu za adui chini ya ardhi
Wapandaji walipoamka asubuhi hawakuona dosari yoyote
Umewahi kujikuta jambo limeharibika nyumbani mwako, kanisani, maishani mwako lakini haijulikani lilianza lini kuharibika
Walipoamka asubuhi bila shaka walienda kumwagilia bila kujua kwamba wanamwagilia na mbegu za magugu
Sio tu adui alipanga mabaya kwa ajili ya ngano lakini pia alipanga kuzitumia nguvu na gharama za wapandaji na mwenye shamba kuotesha na magugu
Walipomwagilia hawakuona dosari yoyote hadi zilipoota.
Huo ndio wakati mfumo wa mizizi ulikuwa unajengwa. Kadri walivyomwagilia ngano ndivyo walivyomwagilia magugu kiasi ambacho mtandao ukawa mfumo kwenye udongo
Kabla mwaka haujaanza, mfumo utakaokusumbua umewekwa
Kabla ya Harusi na ndoa yako mfumo uliwekwa tayari
Kabla ya degree yako mfumo uliwekwa tayari
Kabla ya kuanza uinjilisti ulipomaliza mafunzo mfumo uliwekwa
Kwa hiyo Yesu anaposema nipo pamoja nanyi hata ukamilifu wa dahari katika Mathayo 28:20 na Marko 15:17-20 anamaanisha kwamba unapoinjilisha anatangulia kupambana na mfumo.
Hata ukipuuza haya shetani hatapuuza haya na atakuwekea mfumo
Kila siku mizizi ya ngano na mizizi ya magugu huingilina na kushikana ardhini
Kwa hiyo, Bwana Yesu anaposema “ufalme wa mbinguni umefanana na …” anasema ufalme wa mbinguni umefanana na vita iliyo chini kwa chini kabla haijatokea
Unajaribu kupambana juu ya ardhi (unapigana na damu na nyama), lakini vita unayoiona imewekewa mifumo na miundo mbinu chini ya ardhi (uliwengu wa roho)
Soma tena Waefeso 6:10-12
Mwambie jirani yako “vita unayoiona hapa ina mizizi rohoni”
Twende na mimi kwenye pointi namba tatu;
III. UHARIBIFU NA MAANGAMIZI NI VITU VIWILI TOFAUTI
Adui asingeweza kuua ngano ili isizae ngano na badala yake aliharibu mazingira ambayo kwa ngano ingemea
E Mungu wangu!
Adui alishindwa kukuzuia kuzaliwa lakini aliandaa
Mazingira magumu ya maisha yako
Mwambie jirani, “Adui hawezi kukuua ila atakutesa”
Hawezi kuua hatima yangu
Hawezi kuua kesho yangu
Hawezi kuua ambacho Mungu ameweka ndani yangu
Hawezi kulaani ambacho Mungu amekibariki! Ila jambo moja la uhakika ni kwamba ataharibu mazingira ya hatima yako,
Mazingira ya kesho yako
Mazigira ya maisha yako
Kama mizizi yangu ilibarikiwa na matunda yangu yatabarikiwa
Mchawi hawezi kukulaani
Mapepo hayawezi kukulaani
Kuzimu haiwezi kukulaani
Majaribu unayopitia hayawezi kukulaani
Watakulaani lakini hawafanikiwa kukulaani
Masengenyo yao hayawezi kukulaani
Waambie nimebarikiwa kwenye mizizi yangu, inawezekana huoni aliyonitendea Bwana lakini nimebarikiwa kwenye mizizi
Tangu tumboni mwa mama yangu nimebarikiwa
Uharibifu na maangamizi sio kitu kimoja. Inawezekana maangamizi ni matokeo ya uharibifu lakini sio jambo moja
Adui hawezi kuangamiza baraka zako bali ataharibu mazingira ya baraka zako
Umekuwa ukiomba na kumuuliza Mungu kwanini mambo yako yanarudi nyuma kwa namna yanavyorudi nyuma
Ni kwa sababu kuzimu ilijua umebarikiwa na jambo moja ambalo Adui anaweza kufanya ni kuharibu mazingira kwa kuweka mifumo ya miziz yake kwenye mizizi yako kabla hujashtuka, wakati umelala
Kabla hujaanza kuzaa matunda
Kabla ya kuwepo mwito maishani mwako
Kabla hujapandishwa cheo
Kabla hujaokoka, aliweka mfumo
Na kwakuwa shetani anaamini katika mbegu (Mawazo) kuliko watakatifu wanavyoamini katika mbegu
Watakatifu wangeamini katika mbegu matoleo yasingekuwa shida
Kile ambacho kinasisitizwa makanisani tayari kwenye ufalme kinajulikana kwamba huwezi kuvuna bila kupanda
Wagalatia 6:7-8
2Wakor. 9:6-10
Ukipanda haba utavuna haba
Na ya kwamba mti utautambua kwa matunda yake kwamba ni ngano au ni magugu
Usipoweka chochote hutatoa chochote
Wana wa ulimwengu wanaelewa haya yote na ni vigumu wana wa nuru kuyafahamu kwa sababu wana wa nuru hupanda mbegu mchana wakati adui naye anajifanya wa nuru na hivyo anaona lakini anachopanda adui gizani watakatifu wanakuwa wamelala 2Wakor. 11:7-11
Biblia inasema daima kutakuwa na majira ya mbegu na mavuno
Kila kitu kinatokana na mbegu
Na kama Adui angetaka kuingia kwenye eneo lako angepanda mbegu ya magugu na sio magugu
Shetani anajua unahangaika kufanikiwa bila mbegu ya mafanikio
Usisahau vita viko ardhini
Wapanndaji hawakujua mambo mawili kuhusu magugu
a) Magugu yametoka wapi
b)nia ya adui kupanda magugu kama ambavyo wengi manaosoma aya hii hamjui nia ya adui ilikuwa nini
“Wakamwambia Bwana wao magugu haya yametoka wapi?”
Unajiuliza kwanini najisikia hivi?
Kwa nini nina kichwa kigumu kuelewa vitu?
Kwa nini nimekuwa mzito kanisani?
Kwa nini nimekuwa mwepesi kuangalia mpira
Kwa nini napenda uimbaji kuliko neno la Mungu?
Ni kwa sababu kuna mfumo umetandazwa katika ulimwengu wa roho mahali ambako kuna mizizi yako inayokusaidia kuchipua duniani
Sasa tunajua kuna mtandao wa kimfumo,
Tunajua ni adui aliyepanda mbegu za magugu
Swali ni kwamba;
IV. KWANINI ADUI ALIPANDA MAGUGU WAKATI ANAJUA MAGUGU HAYAUWI NGANO?
Hili ni swali muhimu sana maana usipojua kwa nini shetani amekuwekea hiyo mifumo maishani mwako huwezi kushinda!
Mara ya kwanza nilidhani labda magugu yangeua ngano kwa kuisonga lakini ukweli ni kwamba ngano na magugu vilimea na kukua pamoja hadi ngano kufikia hatua ya mavuno
Kwa sababu kama ilikuwa ngano ilipoenda ardhini itamea ngano
Kama ulikuwa dhahabu unapoingia kwenye tanuru, utatoka ukiwa dhahabu
Na kama wakati inaingia ardhini ilikuwa magugu itamea magugu
Na kama magugu hayakuua ngano, na adui aiwa anajua, kwa nini alipanda magugu?
“Ufalme wa mbinguni umefanana na…”
Kama hawezi kulaani alichokibariki Mungu, kwa nini alipanda magugu tena usiku?
Kama hakuweza kubadili ngano kuwa magugu kwa nini alipanda mbegu za magugu
Kwa nini alijisumbua usiku kwenda kupanda mbegu za magugu pembeni ya kila mbegu ya ngano?
Mfumo haukutesi kwa sababu ya kuwepo magugu na ngano katika huduma yako, maishani mwako, kwenye familia yako, kwenye ndoa yako bali jaribu liko katikati ya ngano na magugu
Jaribu lako liko kwenye maamuzi utakayochukua dhidi ya magugu
Na ndio sababu ya adui kupanda magugu alipanda magugu ili kutega maamuzi ya mwenye shamba. Utanaswa kwenye maamuzi yako
Mtego uko kwenye swali “kwa nini adui alipanda magugu pembeni mwa mbegu ya ngano”
Wapandaji walipouliza kwa nini magugu yapo? Bwana wao alisema “adui amepanda magugu”
Wapandaji hawakujua magugu yalikotoka
Walichojua ni kupanda tu
Bwana wao alijua
Ni kama wapandaji hawakujua adui yao ni nani na anaweza kufanya nini
Wakamwambia “tukayang’oe”
Akawaambia “yaacheni” kwa sababu hata uking’oa magugu, miziz yake imeingiliana na mizizi ya ngano na hivyo uamuzi wa kung’oa magugu ungeua ngano
Adui alijua uamuzi utakaochukuliwa ni kung’oa magugu na waking’oa magugu watang’oa na matumaini yao
Sasa ambacho shetani anataka ufanye
Anataka ujiue mwenyewe!
Shetani anataka ujichukulie maamuzi mwenyewe ukidhani unapambana na maadui kumbe unapambana na mfumo aliokuwekea na ule mfumo umeenda chini na maamuzi ya kupambana nao utakuwa unaua ndoto zako mwenyewe
Utakuwa unaua familia yako mwenyewe
Utakuwa unaua huduma yako mwenyewe
Utakuwa unajinyonga mwenyewe
Mungu ameniambia nikwambie kwamba “nyamaza kimya”
Kukaa kimya kutageuza mtego lakini kupambana na mtego kutakuua
Sijui kama linakusaidia lakini hata kama unaona umevumilia umechoka, nyamaza kimya
Umechnganyikiwa jinsi mambo yanavyovurugika, nyamaza kimya
Umeibiwa wanasubiri upambane na mwizi, nyamaza kimya
Wamekudhulumu wanataka upambane nao, nyamaza
Umechoka na tabia za mwenzio, ukipambana naye utaua familia, utaua ndoto zako, utajinyonga
Shetani ameweka mpangilio wa kimfumo ndio maana tangu umeanza kupambana unapoteza nguvu na afya yako lakini hakuna linalobadilika,
Ukipambana utapata vidonda vya tumbo
Ukipambana utapata presha
Ukipambana wanajua utapambana kisha waripue mfumo waliokuzingira nao
Kunyamaza kwa Waisraeli ndiko kulikomzamisha Farao
Nguvu ya kutopambana na magugu ipo kwenye nayakati na majira
Ule haukuwa wakati wa kupambana na magugu
Wakati na majira ulipofika magugu yalichomwa moto
Inahitaji imani kunyamza
Adui anajua hawezi kukulaani ndio maana anataka kukutumia mwenyewe ili ujiue mwenyewe
Mungu anasema nyamaza kimya
Vita ni vya Bwana!
Shetani hawezi kukuzuia usifanye uinjilisti lakini amekuwekea mtego wa kujitilia mashaka mwenyewe
Uing’oa magugu unang’oa na ngano
Unapojaribu kulitengeneza unaharibu zaidi
Usinaswe na mtego wa kukosa uvumilivu
Imani yako inaonekana katika ukimya na kusema sema ni ishara ukosefu wa imani
Hivi sio vita vyako,
Uamuzi wa kung’oa magugu haukutakiwa kutoka kwa wapandaji bali kwa aliyewatuma
Adui amekuwekea moyo wa haraka na pupa lakini leo nataka nikwambie alichiniagiza mungu nikwambie;
Mbegu unayoweza kupanda wkati unapanda ngano ni wakati. Ukipoteza fedha unaweza kupata zingine tena lakini ukiharibu wakati huwezi kuupata tena. Ukipanda wakati, wakati utakupatia majira ya kupata fedha
Uking’oa magugu utapoteza mavuno ya ngano
Bwana anajua jinsi ya kushughulikia magugu, hayashughulikiwi sasa! ni swala majira na nyakati
Kwa sababu umechanganyikiwa na umechoshwa na hujui hata unapambana na nini
Huelewi kwa nini unapambana
Huelewi hata vita yenyewe ilivyoanzaje
Adui anataka ufanye maamuzi na hujui ni maamuzi yapi hayatakudhuru
Mungu anasema usifanye uamuzi wowote kwenye hali hiyo. Tulia nyamaza kimya.
Kukaa mimya hujakosea, ni kusema huu sio wakati wa kufanya maamuzijuu ya magugu
V. MAVUNO HAYAHARAKISHWI NA DHARULA YA MPANDAJI
Mavuno yatakuja.
Haifai kung’oa magugu kabla ya mavuno ya ngano
Ukiyang’oa kabla ya mavuno, unaua mavuno
Majira uliyonayo sio ya kung’oa lakini kuna majira ya kung’oa yanakuja. Kwa sasa nyamaza
Majira yakifika utang’oa bila kusababisha hasara
Mungu ameniambia ni kwambie kwamba unaelekea kwenye nyakati za mavuno
Na kinachofanya uchanganyikiwe ni magugu kuonekana hayavumiliki wakati umeyavumilia miaka yote hii
Hayavumiliki kwa sababu kadri mavuno yanapokaribia ndivyo magugu yanavyorefuka na kuonekana kuliko ngano. Ndivyo ukweli unavyofichwa chini ya majungu na uongo na uzushi
Unakaribia kuvuna ngano
Kanuni ya Mungu inasema “unapanda kwa machozi unavuna kwa furaha”
Hakuna njia nyingine ya kuvuna isipokuwa kwa furaha ndio maana adui anataka usivune ili ukose furaha
Anataka kukupokonya furaha yako
Nyakati ambazo unataka kujitetea, nyamaza kimya
Jambo gumu kulifanya ni kunyamza wakati adui anapokufanya ulipize
Kuna mashambulizi mengine yanakujia ukiwa kwenye njia sahihi na njia bora ya kushughulika nayo ni kutokushughulishwa nayo
Kwa sababu:
1. Sio majira ya kung’oa
2. Ni mtego
Nyamaza ukimtwika Yesu mafadhaiko yako yote
Omba na kufunga ili Mungu akupe ujasiri wa kungoja
Haraka unayoisikia ndani yako inakuingiza kwenye mtego
Umepitia mengi yamekukondesha
Adui hakupanda magugu ili avune magugu. Kwa hiyo hana faida na magugu ila anataka usivune ngano
Ataitumia pupa uliyonayo kukukosesha mavuno
Unatakiwa uelewe kwamba Adui hawezi kukulaani ila anaweza kukutumia ili ujilaani mwenyewe
Hasira zako, ulimi wako vinaweza kulaani ambavyo ni baraka zako
Adui anajua silaha kubwa aliyonayo dhidi ya watu wa Mungu ni watu wa Mungu
Sila ya adui juu ya maisha yako ni maisha yako
Silaha ya adui juu ya familia yako ni familia yako
Silaha adui juu yako ni wewe mwenyewe
Kama huwezi kupata furaha sasa hutapata furaha tena
Baadhi yenu Mungu amewavusha na korona
Kumbuka Wakati ni kila kitu
Adui asikupumbaze kufanya maamuzi mabaya
Jenga imani kwa Mungu.
Atakamilisha alilolianzisha ndani yetu
Hujasahauliwa, hujaachwa
Najua inatishakuzungukwa na magugu
Lakini nikutie moyo, hakuna silaha itakayofanikiwa dhidi yako
Amini tu ngano itakuwa mkate
Mavuno hayachelewa kama mtego utakavyokuchelewesha
Usiziamini hisia zako
Mwonyeshe Ibilisi ajue kwamba ulienda aridhini ukiwa ngano na utatoka kama ngano
Mbegu-ngano-mkate
Sitaacha mpaka nione tumaini la wito wangu
Nakuombea siku zote kwamba;
Roho ya uvumilivu iwe juu yako
Roho ya manung’uniko na malalamiko ikome
Ukimya na ujasiri vikawe nguvu yako
Nguvu haiko katika kelele
Kwa Jina la Yesu Kristo!
Sijui hatima yako ni nini
Sijui Mungu amekuandalia nini
Lakini ninachojua ni kwamba kama Mungu asingekuwa na makusudi na wewe wangekumeza ungali hai kwa jinsi walivyo na chuki hata kama unawasaidia
Acha manunguniko
Ishi kama vile hakuna vita
Pumua, hema!
Amani iwe juu yako
Subira iwe juu yako
Unakaribia kuvuna kuliko ilivyowahi kuwa maishani mwako
Wakati wa mavuno ndipo utakapotenganisha ngano na magugu
Adui anapotaka kukutumia kujiua wewe tumia subira kama silaha ya kuua mbegu za adui kwenye familia yako, kwenye huduma yako, kwenye biashara yako, Kwenye maisha yako
Lakini wewe ni nani kwenye huu mfano?
Wewe ni nani?
1. Watumwa waliopanda
2. Mbegu njema
3. Adui
4. Magugu
Barikiwa!